Nakukaribisha katika Blogu ya Akida uhabarike kwa habari za Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani zilizotokea na zitakazotokea... 'be the First to know..!
Friday, July 31, 2009
'Happy Birthday to us....'
Fadhili na Upendo wakikata keki kwa ajili ya kulishana...
Fadhili akimlisha Upendo keki baada ya kuikata...
Na sasa Upendo anamlisha Fadhili keki...
Na sasa wanamlisha bosi wao, Mkumbwa Ally...
Waoo... huyu ni nani? je, wamjua? ni brother Michuzi akiwalisha keki wadogo zake Fadhili na Upendo...
Waooo... huku ni kitengo cha IT... na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa... ni kuserebuka tu... uhuu!!
Leo ni siku muhimu sana kwetu.. nilikuwa natamani siku moja nikutane na mtu ambaye siku yetu ya kuzaliwa inafanana lakini sikuwahi kubahatika... Upendo Hartsuiker, mwandishi wa Jarida la Star Magazine la Dailynews ndiye wa kwanza kumbaini kuwa siku yetu ya kuzaliwa inaangukia pamoja. Nimefurahi sana kuona hivyo... leo tumekata keki pamoja ya siku yetu ya kuzaliwa na kuwalisha wafanyakazi wenzetu pamoja na bosi wetu, kwa kweli tulifurahi na pia wenzetu walifurahi pia... "Happy birthday to Upendo and me... let's stay for longer lasting.. God bless us"
Monday, July 20, 2009
Wanafunzi Kairuki wagomea ongezeko la ada
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert KAiruki wamegomea ongezeko la asilimia 25 ya ada lililowekwa na uongozi wa chuo hicho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa Serikali ya wanafunzi hao wamesema kuwa ongezeko hilo linawanyima haki ya kupata elimu kutokana na uwezo wao kifedha pamoja na wanaowafadhili kuwa ni mdogo.
Pia wamesema si jambo la kiungwana kwa uongozi huo kusubiri bajeti ya seikali ya mwaka huu 2009/2010 kupitishwa ndipo waongeze kiwango hicho cha ada kwani wafadhili wao ikiwamo Serikali watashindwa kumudu gharama hizo.
Baadhi ya wanafunzi hao wakiwa nje ya majengo ya chuoni kwao wakijadili ongezeko hilo la ada...

Thursday, July 16, 2009
Uchafu Kariakoo mwendo mdundo...
Siku chache baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuripoti habari za kuondolewa kwa taka zilizokuwa zimerundikana katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, blog hii imeshuhudia kurejea kwa taka hizo kwa kasi katika makutano ya mtaa wa Congo na Aggrey leo mchana.
Wafanyabiashara pamoja na wakazi wa jiji hili walionekana kuendelea na shughuli zao kwa tabu juu ya mrundikano wa taka hizo ambazo zilikuwa zikitoa harufu kali na kusababisha kero kwa wapita njia.
Mkazi wa jijini akijaribu kupunguza taka zilizokuwa zimerundikana eneo hilo na kuwa usumbufu kwa wafanyabiashara na wapita njia

Monday, July 13, 2009
Mdau katika pingu za maisha
Nilikuwa nahesabu miezi, ikawa masiku sasa na hatimaye yakabaki masaa, mwishowe zikabaki dakika na sekunde... ilipotimu saa mbili za usiku baada ya swala ya ishaa mambo yakawekwa hadharani... Sheikh aliniambia nimshike mkono baba mkwe na tendo la kufunga ndoa likawadia... "Mimi Fadhili bin Akida, namuoa Shufaa binti Kombo Sweid kwa mahari tuliyokubaliana..." Sheikh ndiye aliyekuwa akitamka maneno hayo na kuniambia nami niyatamke... ikawa hivyo na maneno mengine na punde mambo yakawa yamekamilika.
Bila shaka nimeoa... Sasa siyo tena 'bachela' kama mama zangu wadogo walivyozoea kunitania hapo awali... Sasa siyo tena 'muhuni' kama baba yangu mdogo 'Seif Luwinzo' alivyozoea kunitania hapo awali... Sasa sitokawia tena kurudi nyumbani usiku wa manane kama ilivyokuwa hapo awali... Hakika nimeyaanza maisha mapya kabisa ambayo nilikuwa nikiyatamani wakati wa utoto wangu... Nilipokuwa mtoto nilitamani siku moja na mimi niwe mkubwa na kisha kuitwa baba kama nilivyokuwa namwita baba yangu enzi za utoto wangu... Hii ni hali ya kawaida ambayo wengi wenu mlishaipitia mkiwa watoto.
Fungate limekwisha sasa nimerudi kazini nawajibika huku nikiwa na fikra za nyumbani kwa mke wangu... Namuwaza mke wangu, nafikiria leo atapika nini... wakati mwezi mmoja kabla siku kama ya leo sikuwa na fikra hizi... ama kweli mambo yanakwenda yakibadilika... na siku hazigandi... ah!
Rafiki zangu na wafanyakazi wenzangu wananipa hongera nimeoa... Ahsante Mungu na namuomba anipe maisha mazuri ya ndoa na mke wangu... atuepushe na mabalaa... atufungulie milango ya neema... Amin!
Karibuni tena wasomaji wangu katika blog hii... mambo yanaendelea kama kawaida... utahabarika zaidi ya hapo awali...
Subscribe to:
Posts (Atom)