Tuesday, March 29, 2011

DK SHEIN ATAWAZWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU ZANZIBAR 'SUZA'

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein leo ametawazwa rasmi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, SUZA, katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Majestic mjini Unguja.

Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio hilo:



Baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye maandamano kuelekea eneo la tukio.



Dk. Shein akikabidhiwa kabrasha la vifungu vya sheria vinavyomuwezesha kuwa Mkuu wa chuo hicho



Sasa ni muda muafaka! Dk Shein akivishwa joho kama ishara ya kuwa Mkuu wa chuo hicho baada ya kutawazwa rasmi

PHOTO/SOURCE: STATE HOUSE, ZANZIBAR

DK BILAL AKAGUA MASHAMBA YA MPUNGA YA MTO WA MBU

Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal leo ameingia kwenye siku ya tatu ya ziara yake katika mkoa wa Arusha ambapo anatembelea miradi mbalimbali kwa lengo la kuikagua pamoja na kuizindua mingine.

Miongoni mwa miradi aliyoizindua ni pamoja na ujenzi wa Maabara ya Shule ya Sekondari ya Nanja, wilayani Monduli.

Leo Dk Bilal ametembelea mashamba ya mpunga yaliyopo kwenye mabonde ya mto wa Mbu, wilayani Monduli pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la maabara ya Shule ya sekondri Nanja, wilayani Monduli. Zifuatazo ni picha mbalimbali zinazoonyesha matukio hayo:



Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima kukagua mashamba hayo



Dk Bilal akiangalia mashamba hayo



Dk Bilal akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la maabara ya shule hiyo. Wa mwisho kabisa ni Mbunge wa wilaya hiyo, Edward Lowassa

RITA KUANZA KAMPENI YA KUSAJILI VIZAZI NA VIFO



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini nchini (RITA), Fillip Saliboko (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo kuhusu Kampeni ya Usajili wa Vizazi na Vifo kwa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Mwingine ni Mkurugenzi wa Haki za Kisheria (DLRP), Emmy Hudson

PHOTO/SOURCE: YUSUF BADI

JK AKABIDHIWA RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI



Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali na mashirika yake Ikulu, Dar es Salaam jana

PHOTO/SOURCE: STATE HOUSE

MWAKILISHI WA NAKAYAMA AKAGUA MAENDELEO SEKONDARI YA WAMA-NAKAYAMA

Rais wa Shirikisho la Uchumi na Maendeleo kwa nchi za Afrika (AFRECO) ambaye pia ni Mwakilishi wa Nakayama kutoka nchini Japan, Seneta Tetsuro Yano leo ameitembelea Shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama iliyopo Nyamisati mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya shule hiyo.

Zifuatazo ni picha mbalimbali zinazoonyesha ziara ya Kiongozi huyo akiwa na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete


Seneta Yano akikabidhi madaftari kwa walimu wa shule hiyo. Kulia ni Mama Salma Kikwete


Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wenye tabasamu wakati wa ugeni wa kiongozi huyo


Seneta Yano na Mama Salma Kikwete wakiwa darasani


Seneta Yano akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi, walimu na wanafunzi wa shule hiyo

PICHA: MAELEZO

UTEPE MWEUPE WATOA SOMO LA UZAZI KWA WABUNGE


Mratibu wa Muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama nchini, Rose Mlay akielezea jambo kwa wenyeviti wa kamati mbalimbali za bunge za kudumu pamoja na wajumbe, wakati wa mkutano kuhusu hali ya uzazi nchini uliofanyika Dar es Salaam jana.

Katika mkutano huo mada mbalimbali zinazohusu uzazi salama kwa Mama mjamzito na mimba za utotoni ziliwasilishwa.

NEMC YATOA MILIONI 15 KWA VIKUNDI VYA MAZINGIRA

Baraza la Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC), leo asubuhi limekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa vikundi vya mazingira kutoka mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Mara na Morogoro kwa ajili ya kusaidia kuendeleza miradi ya mazingira katika maeneo yao.

Vikundi hivyo ni Angaza Women cha Siha mkoani Kilimanjaro, Watu Maji na Mazingira (WAMAMA) cha Tarime mkoani Mara pamoja na Kilombero Group for Community Development (KGCD) ambavyo kila kimoja kimepata shilingi milioni 5.


Wawakilishi wa vikundi hivyo, (Kutoka kushoto) Christina Kulunge wa Morogoro, Lucas Bwana wa Tarime na Mama Mchungaji Joyceline Njama wa Kilimanjaro kwa pamoja wakiangalia mfano wa hundi yao waliyokabidhiwa leo na NEMC