Monday, August 1, 2011

LAGHAI MZOEFU ANASWA MTAA WA KONGO

Usithubutu kusimamisha gari lako pindi akufuatapo na kuanza kukwambia umemgonga! Kitakachofuatia ni kukupora kila kitu kilichomo kwenye gari lako. Huyu ni laghai mzoefu aliyekuwa amefumbiwa macho na wafanyabiashara wa Mtaa wa Kongo jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Nurdin. Lakini waswahili wanasema za mwizi arobaini. Leo amenaswa kweupeee na mgambo wa jiji akitaka kumlaghai dereva wa teksi mtaani hapohapo! Fuatilia tukio zima katia 'series' ya picha


Ilianza hivi... Hawa ni Mgambo wa jiji wapo kwenye Patrol yao...


Ghafla wanamkuta 'Nurdin' akiwa amemzuia dereva wa teksi akidai kagongwa...


Mgambo wanashuka ili kujua nini kinachoendelea...


Mgambo baada ya kuhoji na kuambiwa 'Nurdin' ni laghai na ndio staili zake, wanamkwida na kuondoka naye...


Wanamdhibiti kisawasawa ili kumpandisha kwenye gari lao...


'Nurdin' anapingana nao na kuanza kuleta kashkash...


Lakini nguvu ya 'Teja Nurdin' ni ya kitoto sana kwa mgambo hawa... wanampandisha sasa kwenye gari lao...


Hapa amedhibitiwa kisawasawa akiwa ndani ya gari la mgambo hawa...


Hebu 'cheki' sura hii ukiambiwa ni kibaka na tapeli mzoefu utakataa? Mgambo haoooo wanaondoka na Nurdin...

FOLENI BADO YAWATESA WAKAZI DAR


Magari yakiwayamesongamana kwenye Mtaa maarufu wa Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam kama ilivyonaswa na kamera ya sponsor leo mchana. Foleni ya magari bado ni kero inayowatesa wakazi wa jiji hilo.

FIFA YAENDESHA MAFUNZO KWA MAKOCHA WANAWAKE


Mkufunzi wa mafunzo ya ukocha kwa wanawake wa FIFA kutoka nchini Namibia, Jacqueline Chipanga akielekeza jambo kwa makocha hao kutoka mikoa mbalimbali nchini wakati wa mafunzo hayo yaliyoanza leo kwenye hoteli ya Rainbow, jijini Dar es Salaam.

WASHINDI TIGO JIPANGE KIMAISHA WAKABIDHIWA MILIONI 5


Washindi wa promosheni ya Jipange Kimaisha inayoendeshwa na kampuni ya simu ya Tigo (kutoka kushoto) Festo Saluni, Jane Mtenga na Nasoro Muharam wakiwa wameshikilia hundi yao ya shilingi milioni 5 mara baada ya kukabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.

KOICA YANOGESHA NANENANE MOROGORO


Balozi wa Korea Kusini nchini, Kim Young- Boon (kushoto) akiwa amebeba mgongoni kifaa inachoitwa ‘Jige’ ambacho hutumiwa na wananchi hasa wakulima vijijini nchini Korea Kusini kwa urahisi mara baada ya kufungua Banda la Koica leo mjini Morogoro kwenye Maonesho ya wakulima yaliyoanza kwenye viwanja vya Nanenane mjini humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kanali Mstaafu Issa Machibya.
Picha: John Nditi