Friday, February 24, 2012

SUMBAWANGA YAZINDUA KAMPENI YA USAFI ‘SUMBAWANGA NG’ARA’


MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akimwongoza Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal katika eneo la mkutano wa hadhara mjini Sumbawanga ambapo alisalimiana na wananchi na badaye alizindua kampeni ya kuuweka safi mji wa Sumbawanga iitwayo 'Sumbawanga ng'ara".


Mama Asha Bilal akimsalimia mtoto Juma Kapele(08) mlemavu wa ngozi 'albino' alipotembelea kituo cha kulelea watotot yatima kinachomilikiwa na kanisa katoliki cha Mtakatifu Martin de Pore kilichpo katika eneo la Katandala mjini Sumbawanga, mtoto Juma alipokelewa mawaka jana na kituo hicho baada ya kutoroshwa na mtu ikidaiwa kwa imani za kishirikina ambapo baada ya siku tatu aliokotwa porini akiwa ametelekezwa lakini alikuwa amepingwa chale mwili mzima


MKuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi vifaa vya usafi Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal ili naye awakabidhi kikundi kinachofanya usafi katika mjini huo wa Sumbawanga muda mfupi kabla dk Bilal hajazindua kampeni ya usafi maarufu kama "Sumbawanga ng'ara"

source: Peti Siyame

MAMIA WAMUAGA MAMA MZAZI WA BLANDINA NYONI

Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwemo viongozi mbalimbali wa ngazi za juu Serikalini wamejitokeza kwenye ibada ya kumuaga Mama mzazi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni, Mama Ester Nyimbo Badi katika Kanisa la Azania front jijini.

Marehemu Ester Nyimbo Badi alisafirishwa leo kwenda Iringa kwa mazishi.



Mwili wa Mama Ester Nyimbo Badi ukiingizwa kwenye gari maalumu kwa ajili ya kusafirishwa kwenda iringa kwa mazishi.

source: Courtesy of Badi

JK AWASILI BOTSWANA KUHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA CHAMA TAWALA CHA NCHI HIYO


Rais Jakaya Kikwete akipokewa na Rais wa Botswana, Jenerali Seretse Khama Ian Khama baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Sir Serese Khama jijini Gaberone, Botswana, leo February 24, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pia athudhuria sherehe za miaka 50 ya Chama tawala cha Kidemokrasia cha Botswana 'Botswana Democratic Party'


Rais Jakaya Kikwete akitazama ngoma za asili ya Watswana kutoka kundi la Makhirikhiri


Rais Jakaya Kikwete akiwaslimia wananchi wa Botswana.

PINDA AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA KIJAMII SHINYANGA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama joko banifu kwenye jiko la shule ya sekondari ya Kishapu akiwa katika ziara ya mkoa wa Februari 23, 2012.


Askari wa Jeshi la Jadi yaani Sungusungu wa mji mdogo wa Maganzo wakicheza ngoma yao wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara katika mji huo mdogo akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 23,2012.


4995 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kishapu wakicheza ngoma wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipofungua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 23, 2012.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaaga kwa kuwapungia wananchi wa Mji Mdogo wa Maganzo baada ya kuwahutubia akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 23, 2012.

source: PMO

DKT BILAL AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA KIJAMII KATIKA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Luteni Godfrey Semiono (Mkuu waKambi) kukagua kikosi cha Ulinzi wa Mipaka cha Kasanga kilichopo katika kijijicha Lusambo, pembezoni mwa Wilaya ya Sumbawanga, wakati alipofika eneo hilo kwaajili ya kuzindua maghala ya kuhifadhia bidhaa katika Bandari ya Kasanga janaFebruari 23, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa.


Makamu wa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuwaagawananchi wa Kijiji cha Lusambo waliojitokeza katika mapokezi yake alipofikakuweka jiwe la msingi katika Soko la Kasanga, akiwa katika ziara yake ya Mkoawa Katavi na Rukwa jana februari 23, 2012.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea kukagua maeneo ya kufanyia biashara ya baadhiya wafanyabiashara wa samaki katika Soko la Samaki la Kasanga, baada ya kuwekajiwe la msingi katika soko hilo akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi naRukwa, jana Februari 23, 2012.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika moja ya jengo kati yamawili ya Maghala ya kuhifadhia Bidhaa yaliyopo katika Bandari ya Kasanga,kijiji cha Lusambo Wilaya ya Sumbawanga, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoawa Katavi003 na 004:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea kukagua maeneo ya kufanyia biashara ya baadhiya wafanyabiashara wa samaki katika Soko la Samaki la Kasanga, baada ya kuwekajiwe la msingi katika soko hilo akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi naRukwa, jana Februari 23, 2012.

Thursday, February 23, 2012

MAN U YAPIGWA 2-1 NA AJAX NYUMBANI


Mchezaji wa Manchester United, Phil Jones (kushoto) akiwania mpira na Aras Ozbiliz wa Ajax katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya raundi ya 32 uliochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester usiku huu.

Ozbiliz aliisawazisha goli timu yake ya Ajax Amsterdam dakika ya 37 baada ya Hernandez kuifungia timu yake ya Manchester United goli la kuongoza katika dakika ya 6 ya kipindi ch kwanza.


Alderweireld akaongeza bao la ushindi dhidi ya timu yake ya Ajax katika dakika ya 87 ya kipindi cha pili cha mchezo na mpaka dakika 92 za mchezo kuisha Ajax walitoka vifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester United.

Manchester United ilishindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford wakati wa mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulya (UEFA) iliyomalizika hivi punde.

Source: eurosport

CAMERON AONYA USALAMA WA DUNIA UPO MIKONONI MWA SOMALIA



Waziri Mkuu wa Uingereza, Davida Cameron amezitaka Jumuiya za Kimataifa kumaliza kwa haraka machafuko nchini Somalia hususan suala la uharamia vinginevyo taifa hilo la Afrika litakuwa tishio duniani kwa ugaidi.

Viongozi wan chi mbalimbali duniani wamekutana jijini London, Uingereza kutafuta njia za kumaliza matatizo mbalimbali nchini Somalia vikiwemo Ugaidi, Migogoro pamoja na Utawala dhaifu vinavyoendelea nchini humo.

Nchi 40 ikiwemo Tanzania zinahudhuria mkutano huo unaoendelea Lancaster House jijini London, Uingereza.

source: CNN

ITALIA YALAUMIWA KUKIUKA HAKI ZA WAAFRIKA

Mahakama ya Ulaya kuhusu haki za binadamu imetoa uamuzi wake kuwa Italia ilivunja haki za binadamu kwa wahamiaji wa Eritrea na Somalia kwa kuwarudisha tena Libya.

Mahakama ilamuru Italia imlipe kila mmoja wa wahamiaji hao kwenye kesi Euro 15,000 (£13,000; $20,000).

Mwaka jana Italia ilisitisha makubaliano ya mwaka 2008 na Libya wa kuwarudisha wahamiaji nyumbani.

Kitengo cha mahakama (Grand Chamber judgment) katika kesi ya Hirsi Jamaa na wengine dhidi ya Italia kilikuta walalamikaji kuwa wamekwekwa kwenye hatari ya kutotendewa haki nchini Libya na kurejeshwa Somalia au Eritrea.

Hatua hiyo ni ukiukwaji wa kifungu cha tatu cha makubaliano Ulaya kuhusu haki za binadamu kinachozuia uhalifu wa kibinadamu ua kuwawapa haki yao.

Kulikuwa pia na ukiukwaji wa wa kifungu cha Nne kinachozuia urejeshwaji wa pamoja, kwa mujibu wa makubalino ya hukumu ya majaji.

Hukumu ya Mahakama ya Juu ni ya mwisho ikimaanisha kuwa kisheria imeifunga Italia.

Mahakama ilisema kuwa mwaka 2009 Italia ilifanya operesheni tisa baharini kuzizuia boti za wahamiaji, kulingana na makubaliaono yaliyotiwa saini na waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi na kiongozi wa Libya wakati huo marehemu Kanali Muammar Gaddafi.

Februari 26 mwaka jana Italia ilitangaza kusitisha makubaliano yake baada ya machafuko ya Libya.

source:BBC

TANZANIA YASAINI MAKUBALIANO YA UBADILISHANAJI MAHARAMIA NA UINGEREZA




Rais Jakaya Kikwete na Waziri masuala ya Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa na Afrika na Mazingira (Parliamentary Under Secretary responsible for Africa, United Nations, economic issues, conflict resolution, and climate change) wa Uingereza, Hendry Bellingham wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe akiweka saini sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo mbili juu ya taratibu za kukabadhiana watuhumiwa wa uharamia na mali zilizokamatwa katika matukio ya uharamia katika bahari kuu leo huko Lancaster House, jijini London.

Source: Ikulu

TBL KUANZA KUTUMIA NEMBO MPYA


Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto), akipokea mfano wa nembo ya mistari kwenye bidhaa ya Tanzania (BARCODES) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF), Godfey Simbeye katika uzinduzi wa nembo hizo, Dar es Salaam jana. TBL ni moja ya kampuni kubwa nchini itakayoanza kutumia nembo hizo za Tanzania zinazotengenezwa na kampuni ya GSI Tanzania National Limited.


Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto), akizungumza baada ya kupokea mfano wa nembo ya mistari kwenye bidhaa ya Tanzania (BARCODES) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF), Godfey Simbeye katika uzinduzi wa nembo hizo, Dar es Salaam jana. TBL ni moja ya kampuni kubwa nchini itakayoanza kutumia nembo hizo za Tanzania zinazotengenezwa na kampuni ya GSI Tanzania National Limited.

Source: Courtesy of TBL

JK AWASILI LONDON KUHUDHURIA MKUTANO WA KUJADILI HALI YA MACHAFUKO SOMALIA




Rais Jakaya Kikwete akiwasili Lancaster House, jijini London leo kujiunga na viongozi wa nchi mbalimbali katika mkutano wa kujadili mustakabali wa hali ya machafuko nchini Somalia ambayo imekuwa katika misukosuko kwa zaidi ya miaka 20. Jumuiya ya Kimatifa ikiongozwa na Uingereza imedhamiria kumaliza matatizo mbalimbali katika nchi hiyo ikiwemo kutokuwa na Serikali inayoeleweka, Uharamia, Ugaidi pamoja na kujaribu kurudisha amani.

Source: Ikulu

WAZIRI SAMIA SULUHU ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO ZANZIBAR


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu upakuaji wa makontena katika bandari ya Zanzibar kwa Mkuu wa Mipango (ZPC), Ali Haji Haji wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo mjini humo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Msanifu Haji Mussa na Maofisa wa Bandari ya Zanzibar.




Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samia Suluhu Hassan akitembelea Bandari ya Zanzibar wakati wa ziara yake ya kuangalia shughuli za Maendeleo mjini humo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa bandari, Msanifu Haji Mussa na Maofisa wa Bandari Zanzibar.

Source: VPO

DK BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA CHA MZINDAKAYA


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kuhusu uchinjaji wa ng’ombe na matayarisho yake hadi kufikia nyama kamili kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka, wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt.Mzindakaya, kilichopo Sumbawanga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi naRukwa jana.


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kuhusu vipimo vinavyotumika kabla ya ng’ombe kuchinjwa kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt. Mzindakaya kilichopo Sumbawanga wakati akiwa kwenye ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana.


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kuhusu matayarisho na ufungaji wa nyama katika mifuko tayari kwa kuuzwa kwa wateja kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt. Mzindakaya kilichopo Sumbawanga, wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana.


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi baada ya kuwasili kwenye kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Sumbawanga jana wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa.

Source: VPO

REDDS YATOA ZAWADI ZA WAPENDANAO


Balozi wa kinywaji cha Redds Original Akimkabidhi kifurushi cha zawadi mbalimbali Mkurugenzi wa kampuni ya ASSET Entertainment, Asha Baraka kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wapendanao Duniani.


Balozi wa kinywaji cha Redds Original akimkabidhi zawadi mbalimbali toka Redds, Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania, Angella Msangi kwa niaba ya Uongozi wa Shirika hilo kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Wapendanao Duniani.


Mmoja kati ya Mabalozi wa kinywaji cha Redds Original akimkabidhi kifurushi cha zawadi mmoja kati ya wateja na washirika wa kinywaji hicho hivi karibuni kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Wapendanao Duniani.

Source: Courtesy of Redds Original

Wednesday, February 22, 2012

WAKRISTO NA IBADA YA MAJIVU ST. JOSEPH KUJIANDAA NA PASAKA




Sista Anthonia Samba wa Kanisa la Mt. Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam akiwapaka majivu waumini wa dini ya Kikristo kuashiria Jumatano ya Majivu jijini leo. Waumini wa dini ya Kikristo wameanza kufunga kwa resima kujiandaa na Sikukuu ya Pasaka.

source: Okanda

MAUAJI SONGEA YAFIKIA WATU 10, FFU WAFYATUA RISASI NA MABOMU KUTAWANYA MAANDAMANO


Askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakiondoa mkokoteni uliowekwa barabarani na vijana walioandamana katika eneo la lizaboni Manispaa ya Songea.


FFU wakiondoa magogo yaliyowekwa barabarani na vijana wa lizaboni kupinga wenzao kuuawa na watu wasiojuklikana katika maeneo mbalimbali mjini Songea.


FFU wakiwa na mmoja kati ya vijana aliyeshiriki maandamano haramu mjini Songea kupinga mauaji ya raia yanayoendelea mjini humo ambapo hadi sasa watu 10 wameshauawa na watu wasiojulikana.


FFU wakimshikilia mmmoja wa vijana waliokuwa wakiwarushia mawe katika mapambano kati ya polisi na baadhi ya wakazi wa Songea.


FFU wakiwa na vijana walioshiriki maandamano haramu katika manispaa ya songea kupinga mauaji ya wenzao hasa madereva wa pikpiki yanayoendelea mjini humo.


Mkuu wa Wilaya ya Songea ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Thomas Sabaya akizungumza wakatika wa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa ruvuma kushoto ni Mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu.


Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Said Mwambungu (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa baada ya kutokea mauaj ya vijana 3 na maandamano kati ya FFU na vijana hao.


Watendaji wa mitaa na Wenyeviti wao wakiwa katika mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Mwambungu wakati wa kikao cha dharura kujadili namna ya kukomesha mauaji ya watu wasio na hatia yanayoendelea katika manispaa ya Songea.

SOURCE: MUHIDINI AMRI/ SONGEA

MUUZA DVD KAMA AL-SHABAAB AU BOKO-HARAM

Huyu si Al-Shabaab wala Boko-Haram, la hasha, ni kijana Idrissa Sadiki Nyambo mkazi wa Mabibo Hostel, jijini Dar es Salaam ambaye ameamua kutoka na ‘staili’ ya aina yake ya kufanya biashara yake ya kuuza dvd.

Idrissa anasema kuwa ‘staili yake hiyo imemfanya apate wateja wengi kwa muda mfupi kwani wateja hao hutaka kujua anabeba vitu gani vya ziada na kwa nini avae hivyo. Ndipo hapo wanapojikuta wamenasa na kuanza kununua dvd zake.


Ustadh Idrissa Sadiki Nyambo akipita kutafuta wanunuzi

Anasema kuwa kwa siku mauzo yake hufikia 50,000/- na wakati mwingine hadi 80,000/-.

Huu ndiyo ubunifu ambao Idrissa Sadiki ameufanya na kujikuta maisha yake yanamwendea vizuri.


Mdau akichagua dvd kwa Ustadh Idrissa Sadiki Nyambo

MBABE ANAPOKUTANA NA MBABE MWENZIE..

Hii ilikuwa mitaa ya Ubungo Riverside jirani na darajani, jamaa anayedaiwa kuwa mbabe wa kuzuia watu kupita njia alipopewa 'kibano' cha haja na mbabe mwenzie baada ya kukerwa na vitendo vyake.

Kamera ya blogu hii ilipofika eneo hilo ilikuta mtifuano huo ambao ulianza kama muvi vile. Jamaa huyo ambaye jina lake halikuweza kupatika mara moja alikuwa akiwazuia watu kupita kwenye 'kamlango' kanakounganisha wakazi wa Ubungo Maziwa na Riverside.

Inadaiwa jamaa huyo alikuwa akimzuia kila anayepita hapo kwa kudai lazima kwanza atandikwe ngumi mbili au tatu hivi (yaani mpitanjia amtandike huyo jamaa) mpaka atakotosheka ndipo amruhusu. Ni jambo la kushangaza kwa kweli, lakini imetokea.

Baadaye vurugu iliibuka baada ya mmoja wa wapitanjia hao kukataa na ndipo 'mbabe' huyo akaanzisha vurugu kabla hajatiwa nguvuni na mbabe mwenzie.

Shuhudia tukio hilo katika picha zifuatazo;


Mbabe (kushoto) akimchimba mkwara mpitanjia sipite kwenye mlango huo


Mbabe mwenzie anatokea na kumtia nguvuni


Mbabe anatiwa nguvuni


Hapa ni kama anamwambia 'ukifurukuta nakutandika ngumi'

source: akidasenior