Saturday, February 28, 2009

Tazama matukio tofauti ya mwisho wa wiki katika Picha...

'Ebwanaee, kumbe tamu hivi...' hawa ni wanene wenyewe wa 'BURN' Energy drinking waki'test' kinywaji hicho baada ya kukizindua, Club Billicanas, Dar es Salaam jana...


'Ngoja nisaini fastafasta nikamate mshiko...! Unamjua huyu? anaitwa simba wa vita, Mzee wetu Rashid Kawawa akisaini kitabu chake mwenyeewe alichokitunga... hapa ni baada ya kuzinduliwa na JK, Ikulu Dar es Salaam hivi karibuni... pembeni yake ni mzee wa Ruksa.. Mwinyi


"Mama wala usiwe na wasiwasi... sisi ndio wenye nchi hii, tunajua wapi pa kuingilia wapi pa kutokea... Nakumbuka enzi za mwalimu tulikuwa tuko 'beneti' sana, so we punguza presha maana naona kama unataka kupandisha vile... teh tehe.."


'Ngoja mwanangu nikurekebishe hijabu eenh..., ndivyo anavyoonekana mama huyu akimwambia binti yake wakati wa mahafali ya nane ya shule ya sekondari ya Ridhwaa, Dar es Salaam leo



Baadhi ya washiriki wa shindano la maisha plus wakiwa katika pozi kabla ya kujuchwa ili kuwapata washiriki 18, watakaoingia kijijini....


'tatizo lenu hamsomi...!' Sasa nataka kuanzia sasa mkaze msuli katika masomo yenu... Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, Mwantumu Mahiza akifafanua jambo wakati wa mahafali ya shule ya seminari ya Ridhwaa, Dar es Salaam leo


Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Uingereza, Tanzani, Bi. Diane Louise Corner, Ikulu Dar es Salaam hivi karibuni...


'Unajua bwanamdogo unanikosha sana namna unavyowatia kashkash hawa mafisadi... teh tehe tehee...!

'Haya bwana mzee ngoja nikuzindulie kitabu chako hiki, ukaanze kula vichwa.. teh tehee!' Ndivyo anavyoonekana JK akimwambia simba wa vita, Mzee Rashid Mfaume Kawawa katika uzinduzi wa kitabu hicho, Ikulu Dar es salaam juzi














































No comments:

Post a Comment