Thursday, March 12, 2009

HUKUMU YA ALIEMZABA RAIS MWINYI KOFI KESHO..

Mtuhumiwa katika kesi ya kumshambulia Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Ibrahimu Said 'ustaadh' anatarajia kufikishwa tena Mahakamani kesho kwa ajili ya kusomewa hukumu yake baada ya leo kushindikana.

Awali Ibrahimu ambaye alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo asubuhi alikiri kosa lake mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, jambo lililorahisisha kuifanya kesi imalizike haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kupandishwa kizimbani, Ibrahimu ameiomba mahakama imuachie huru ili akasome na kuongeza kuwa haikuwa dhamira yake kumzabua kofi Rais Mwinyi.

"Naomba mahakama iniachie huru nikasome. Namuomba mzee (Mwinyi) anifutie hii kesi." Alisema.

Wakati huohuo, mama mzazi wa mtuhumiwa huyo, Mama Rehema Ngoma ambaye alionekana kuchanganyikiwa muda mfupi baada ya mwanaye kurudishwa rumande alisema Ibrahimu alipata msukosuko wa ubongo akiwa mdogo jambo linalomfanya wakati mwingine kuchanganyikiwa.


Ibrahimu Said 'Ustaadh' (kulia) akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo

Mama Mzazi wa Ibrahimu Said 'Ustaadh', Mama Rehema Ngoma akizungumza kwa jazba na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mwanaye kurudishwa rumande...

No comments:

Post a Comment