Nakukaribisha katika Blogu ya Akida uhabarike kwa habari za Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani zilizotokea na zitakazotokea... 'be the First to know..!
Monday, May 25, 2009
Thursday, May 21, 2009
MAMIA WAMPOKEA DK MWAKYEMBE
Umati wa ndugu, jamaa na marafiki wa Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe wakitoa machela iliyombeba Mbunge huyo kutoka ndani ya Ndege baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere, kabla ya kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi. Dk Mwakyembe alipata ajali ya gari huko Iringa asubuhi ya leo na kuthibitika kuvunjika taya.
Tuesday, May 19, 2009
MA 'DC' WAPIGWA MSASA
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey Mwanri amewataka wakuu wa Wilaya zote nchini kushirikiana katika kazi zao kwa manufaa ya nchi pamoja na wananchi wake kwa ujumla.
Mwanri alisema hayo wakati wa kikao cha kazi na Wakuu wa Wilaya zote Tanzania Bara kilichofanyika leo Dar es Salaam.
Wakuu wa Wilaya za Kilindi na Kondoa, Halima Mchuka na Betty Mkwasa wakisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha pamoja cha wakuu wa wilaya zote Tanzania Bara leo, jijini hapa.

Monday, May 18, 2009
Flu pandemic may be unfolding: WHO
GENEVA
Humanity may be witnessing an influenza pandemic unfold, the head of the World Health Organization said on Monday, as Japan reported a big jump in infections with the newly-discovered H1N1 virus.
Flu fears dominated the start of the WHO's annual congress in Geneva, where many of the 40 countries touched by the flu strain urged the United Nations agency to rethink its pandemic alert scale that is now at the second-highest notch.
WHO Director-General Margaret Chan said the outbreak that began in North America and has stretched to Europe, Asia and South America needed to be tackled with seriousness even though its symptoms appear to be largely mild.
"For the first time in humanity, we are seeing, or we may be seeing, pandemic influenza evolving in front of our eyes," Chan told the World Health Assembly meeting in Geneva, where rich and poor governments discussed their drug, vaccine and other needs.

'HAPA DIPO ANGUKIA BOMU'
MKAZI wa Mbagala Misheni, mwenye asili ya ki'asia' pamoja na 'dog' wake akiangalia shimo ambamo kuliangukia moja kati ya mabomu yaliyolipuka wiki 3 zilizopita katika kambi ya Jeshi ya Mbagala. Askari wa Jeshi walifika hapo leo kulichomoa bomu hilo ambalo lilikaa hapo kwa zaidi ya wiki 3 pasio kugundulika. Kwa mujibu wa mama huyo amesema bomu hilo lilikuwa na takriban urefu wa meta 3.
Ligi ya soka Wanawake yavutia Karume
Thursday, May 14, 2009
MILIPUKO YA MABOMU- LIPUMBA ATAKA TUME HURU IUNDWE
KUFUATIA kutokea kwa milipuko ya mabomu wiki mbili zilizopita katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kambi ya Mbagala, Dar es Salaam, Chama cha Wananchi, CUF kupitia kwa Mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali iunde tume huru itakayochunguza chanzo cha milipuko hiyo.
Tume hiyo itashirikisha wataalamu wa mabomu toka nchi marafiki na Tanzania zikiwemo Ujerumani, Marekani na nyinginezo.
"Hatuielewi serikali kuhusiana na suala la ulipukaji wa mabomu Mbagala. Iundwe tume huru kutoka nje, ituambie ukweli." Alisema.
Aidha amewataka baadhi ya wafuasi wa vyama wanaotumia nafasi zao vibaya katika ugawaji wa vyakula vya misaada kwa waathirika hao kuacha aliouita ufisadi usio na huruma kwa waathirika wa milipuko hiyo, ambao wengi wao ni mama waja wazito, vikongwe na watoto wadogo.
Lipumba alifanya mkutano na waandishi wa habari leo asubuhi, katika ofisi za makao makuu ya chama chake cha CUF, kuzungumzia ajenda tatu ambazo ni Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Busanda, jimbo la Magogoni pamoja na Milipuko ya mabomu iliyotokea Mbagala wiki mbili zilizopita.
Prof. Lipumba akifafanua jambo leo. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad

Wednesday, May 13, 2009
UCHAGUZI MWINGINE JIMBO LA BIHARAMULO WAJA
WIKI chache baada ya kufariki kwa alyekuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi kwa tiketi ya TLP, Phares Kabuye kufariki dunia, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza rasmi kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa bunge katika jimbo hilo mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Rajabu Kiravu, uteuzi wa wagombea utaanza tarehe 9 mwezi Juni siku moja kabla ya Kampeni za Uchaguzi ambazo zitafanyika tarehe 10 mpaka 4 mwezi Julai, wakati shughuli za upiaji kura zitafanyika siku moja baa ya kumalizika kwa kampeni.
Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Rajab Kiravu

Tuesday, May 12, 2009
HARAKATI ZA KIKOSI CHA JWTZ KATIKA PICHA
HATUNA MPANGO WA KUJENGA KAMBI YA KIVITA YA KIJESHI TANZANIA- MAREKANI
Kamanda wa kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Marekani kwa Afrika, General. illiam Ward amekanusha taarifa kuhusu mpango wa nchi hiyo kujenga kambi ya kivita ya jeshi la hnchi hiyo hapa Tanzania.
General Ward amesema misaada inayotolewa na Marekani kwa Jeshi la Ulinzi la Tanzania haina maana ya kushawishi jeshi hilo kujenga kambi ya kivita ya nchi hiyo hapa nchini, kama baadhi ya taarifa zinavyodai.
General Ward alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari wa Tanzania katika chumba cha mikutano cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ- Makao Makuu), Upanga Dar es Salaaam leo, wakati wa hafla ya kukabidhi magari maalumu ya 'Deraya' yatakayobebea wapiganaji wa kijeshi watakaokwenda Darfur, nchini Sudan hivi karibuni kulinda amani.
"Hizo ni taarifa za kizushi tu." Alisema.
General Ward alisema Marekani na nchi wanachama inafanya juhudi mablimbali za kulinda amani katika nchi za Afrika zilizo katika mizozo ya kivita, na si lengo kujenga kambi za kivita za kijeshi kama inavyodhaniwa na wengi.
Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Uingereza leo walikabidhi magari maalumu yanayojulikana kwa jina la 'Deraya' pamoja na vitu mbalimbali vya kijeshi kwa JWTZ, yatakayosaidia kikosi maalumu kitakachokwenda Darfur, Sudan kulinda amani hivi karibuni.
Jumla ya askari 875 wa JWTZ, wanatarajiwa kwenda Darfur, nchini Sudan kwa ajili ya kusaidia kulinda amani ikiwa ni mkataba wa makubaliano uliotiwa saini na Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, jijini hapa leo.
Katika askari hao, 800 wataingia moja kwa moja katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kusimamia ulinzi na amani katika vituo viwili vya KO-Abeche pamoja na Mujahiriya vyote vya jimbo la Darfur, wakati askari 75 ni wahandisi wa Jeshi ambao watakuwa wakisimamia shughuli zote za ujenzi wa Jeshi hilo litakapokuwa nchini Sudan.
Wakati huohuo, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Lt. General Abdullrahman Shimbo amevitaka vyombo vya habari nchini kutopotosha taarifa zozote zinazohusiana na mambo ya kijeshi kwa wananchi kwa ajili ya kutowapa hofu wananchi hao.
Akizungumzia kuhusu tukio la jana jioni la mlipuko wa bomu, Shimbo alisema bomu hilo lililipuliwa na wanajeshi wa kambi hiyo wakati walipokuwa wakifanya usafi wa eneo la kambi na kukuta bomu dogo la kurusha kwa mkono, hivyo hawakuona sababu ya kuwatia hofu wananchi na kuamua kulilipua, jambo ambalo lilikaririwa tofauti na baadhi ya vyombo vya habari.
"Lile bomu halikulipuka lenyewe. Wanajeshi walililipua baada ya kulibaini wakati wakifanya usafi." ALisema.
Magari ya kijeshi ya 'Deraya' yaliyokabidhiwa kwa JWTZ leo

Sunday, May 10, 2009
Tunaadhimisha vipi Mothers day?
Habari za mchana wasomaji wa blog hii ya sponsor. Bila shaka wengi wenu mpo majumbani na wengine makazini na sehemu mbalimbali za kujipumzisha huku mkidodosa mawili matatu katika mitandao yenu.
Ndio, mambo yamebadilika siku, lazima twende na wakati, siku hizi kupata information ni rahisi kweli kuliko enzi zileee... nadhani mmenisoma. Kwa mtu ambaye atabisha basi huyo mbishi na mvivu totally!
Eh nsije kusahau, hivi leo ni Mothers day vile eenh? Au hata nyie hamjui? Ni kaweli leo ni mothers day. Lakini sasa tunaadhimisha vipi siku hii ya leo? Kwa kuwakumbuka mama zetu, na mama zetu kuwakumbuka sisi watoto zao basi au kuna jingine?
Kukumbukana kupo kwa njia mbalimbali.. kama kupeana zawadi mbalimbali ambazo ni maalumu. Maana wengine zawadi hizi wanashindwa kuzitoa kwa wakati maalumu.
Hebu mpatie mamayo au mwanao kitu ambacho akikitazama, atakuwa anakukumbuka siku zote hata kama utakuwa umeaga dunia. Hizi ni nafasi adimu sana kuzikuta katika maisha yetu. Kwa wale ambao mama zao wameshatangulia mbele ya haki, si mbaya sanana, wakawa wanawatilia ubani au kwa maana nyingine kuwafanyia dua ya kuwaombea heri na amani huko walipo, zote ni aina ya zawadi hizi.
Siku ya leo tuwafanyie mambo mazuri mama zetu, na pia nyiniy mama zetu leo mtupe raha ili kila mmoja wetu ajisikie kwamba kaadhimisha siku ya kina mama yaani 'Mothers day'.

Wednesday, May 6, 2009
Mamia waupokea mwili wa Kiduduye wa redio Uhuru
Mamia ya wakazi wa jijini pamoja na wafanyakazi wa kituo cha utangazaji cha redio uhuru wamefurika katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kupokea mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa kituo hicho, Deogratius Kiduduye ambaye alifariki nchini Nigeria mwishoni mwa wiki.
Dada wa marehemu pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Redio Uhuru wakilia kwa uchungu baada ya kupokea mwili wa marehemu, Deogratius Kiduduye

Tuesday, May 5, 2009
Mkuu wa Majeshi atembelea majeruhi wa mabomu Muhimbili
Monday, May 4, 2009
Albino waadhimisha siku yao leo
TSN Tanga yafunguliwa rasmi
Kampuni ya Uchapishaji Magazeti ya Serikali (Dailynews na HabariLEO), leo imefungua rasmi ofisi yake tawi la Tanga ikiwa ni moja ya malengo ya kampuni hiyo kuwafikia watu wengi zaidi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Joel Bendera akifungua rasmi ofisi za TSN, tawi la Tanga leo jijini humo

Misaada zaidi yatolewa wahanga wa mabomu
MISAADA zaidi imeendelea kutolewa na wahisani mbalimbali kwa wahanga wa milipuko ya mabomu, ikiwasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Leo, Meneja Mkuu wa Kiwanda cha unga cha Bakhressa, Tawi la Mzizima, Said Abeid ametoa msaada wa shs Milioni 100 kwa niaba ya Makampuni ya Bakhresa, ambazo alikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi kwa ajili ya kusaidia wahanga wa milipuko ya mabomu, Mbagala.
Wakati huohuo, Jumuiya ya mabohora wa Tanzania wametoa hundi yenye thamani ya shs milioni 5.2 kwa Mkuu huyo wa mkoa kwa ajili ya kusaidia wahanga hao.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini

Zantel wazindua ZConnect
Kampuni ya simu za mkononi, Zantel leo imezindua huduma ya mtandao kwa wateja wa malipo ya kabla ambayo itaanza kupatikana nchi nzima.
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Fintan Lawler amesema huduma hiyo mpya ya mtandao itaiweka Zantel katika nafasi ya mtoa huduma za kiwango cha juu nchini.
ZConnect ni huduma ya mtandao, data na sauti na watumiaji watapata huduma ya mtandao ya uhakika na kasi.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya simu za mkononi Zantel, Brian Karokola

Sunday, May 3, 2009
ROSTAM: MENGI NI FISADI NYANGUMI
MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz leo asubuhi amevunja ukimya na kumtaja Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuwa ndiye fisadi nyangumi.
Rostam alisema kuwa Mengi anahusika na kuifisidi nchi kwa madai kuwa ndiye aliyehodhi makampuni na taasisi mbalimbali za fedha matokeo yake ameyafilisi na mengi yao kufungwa kabisa.
Rostam amesema kuwa haoni ajabu kutuhumiwa na Mengi kutokana na rekodi aliyonayo ya kulumbana pale anapoona amezidiwa kiushindani katika biashara na yeyote kati ya wafanyabiashara wakubwa hapa nchini.
Mengi ni mmiliki wa vyombo vya habari vya Televisheni za ITV, Channel 5 pamoja na Redio One, East Africa Radio na Kampuni ya the Guardian wachapishaji wa magazeti ya The Guardian, ipashe, Alasiri na mengineyo mengi, wakati Rostam ni mmiliki wa Kampuni ya Uchapishaji wa magazeti ya New Habari, wachapishaji wa Magazeti ya The African, Mtanzania, Dimba na mengineyo.
Aidha amesema kuwa atawasilisha vithibitisho vinavyomuhusu Mengi kuwa ni Fisadi Mahakamani na kumfungulia kesi ya kashfa dhidi yake ndani ya saa 48.
Rostam akionyesha document kwa waandishi wa habari

Subscribe to:
Posts (Atom)