MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz leo asubuhi amevunja ukimya na kumtaja Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuwa ndiye fisadi nyangumi.
Rostam alisema kuwa Mengi anahusika na kuifisidi nchi kwa madai kuwa ndiye aliyehodhi makampuni na taasisi mbalimbali za fedha matokeo yake ameyafilisi na mengi yao kufungwa kabisa.
Rostam amesema kuwa haoni ajabu kutuhumiwa na Mengi kutokana na rekodi aliyonayo ya kulumbana pale anapoona amezidiwa kiushindani katika biashara na yeyote kati ya wafanyabiashara wakubwa hapa nchini.
Mengi ni mmiliki wa vyombo vya habari vya Televisheni za ITV, Channel 5 pamoja na Redio One, East Africa Radio na Kampuni ya the Guardian wachapishaji wa magazeti ya The Guardian, ipashe, Alasiri na mengineyo mengi, wakati Rostam ni mmiliki wa Kampuni ya Uchapishaji wa magazeti ya New Habari, wachapishaji wa Magazeti ya The African, Mtanzania, Dimba na mengineyo.
Aidha amesema kuwa atawasilisha vithibitisho vinavyomuhusu Mengi kuwa ni Fisadi Mahakamani na kumfungulia kesi ya kashfa dhidi yake ndani ya saa 48.
Rostam akionyesha document kwa waandishi wa habari
No comments:
Post a Comment