Thursday, January 28, 2010

TOP TEN HEALTHIEST VEGETABLES

There is no doubt that adding vegetables to your diet at any stage of life can improve your health. Often, people being treated for diseases such as cancer are advised to increase their intake of vegetables to help give their bodies the boost it needs. Here is a list of ten vegetables that are great choices to add to your diet that will improve your health.

1- Collard Greens
Widely consumed in the Southern US for many years, this leafy green vegetable packs a lot of nutrient value. Collard Greens have high levels of calcium, Vitamin E, and beta-carotene. In addition to these nutrients, it also boasts high selenium content. Collard greens can be had throughout the year but most consider them to be best between January to April


2- Sweet Potatoes (Shakarkand)
The anti-oxidant properties of sweet potatoes can help to rid the body of free radicals linked to many chronic illnesses including diabetes and colon cancer. They are also thought to be able to lessen the effects of asthma and arthritis due to their anti-inflammatory tendencies. Sweet potatoes are also a good source of iron, calcium and fiber, and best of all they can be used in a number of recipes.


3-Broccoli (Hari Phool Gobhi)
Like so many vegetables out there, this one is also great protecting your body from the ravishes of cancer. They are attractive enough to enhance any dish but their uses go far beyond aesthetics. With high folic acid levels, it is useful in preventing birth defects. In addition it is great for getting enough calcium and vitamin C in your diet.


4- Onions
This unassuming bulb actually offers more health benefits than you may think. They help to lower blood sugar levels in addition to promoting good cardiovascular health. It has been proven that adding onions to your diet can reduce your risk of developing certain cancers and contribute to gastrointestinal health.


5- Carrots
Ask anyone to name a vegetable, and most of them will say ‘carrot’ right off the bat. There’s a reason why this vegetable is so popular. Apart from being one of the most commonly used, it is the best source of the pro-vitamin A carotenes. They are also known to help strengthen the vision, in particular night vision. Carrots can also be used to regulate blood sugar levels and are good for the health of the colon.


6- Spinach (Paalak)
While most people make a face at the thought of eating this vegetable, but spinach actually protects us from a number of illnesses like arthritis, heart disease and osteoporosis. Studies have shown that spinach contains a minimum of 13 flavonoid compounds. Serious illnesses like ovarian and prostate cancer can also be helped by consumption of spinach.


7- Kale(perhaps saag)
This vegetable has a multitude of benefits for the body. Like every other vegetable it contains important vitamins, but has more dietary value per calorie than most vegetables. Kale is known for its detoxing ability, as well as its proven capacity for reducing the risk of cancer, especially of the ovaries. Consuming adequate amounts of this vegetable can also help to keep lungs healthy. Maybe the best thing about kale is that it can easily be grown in home gardens.


8- Eggplant (baigan, brinjal)
Studies have indicated that eggplant may have a protective effect on the brain. The fact that they are low in calories makes it a popular food among dieters and health conscious individuals. This vegetable has high levels of copper, potassium and fiber. Eggplants positive effect on cardiovascular health is well documented.


9- Cucumbers (kheera),(KAKDI)
Widely acknowledged for its soothing effect on the skin, cucumber is popular not only for eating but skincare products. It has a positive overall effect on the body, including the ligaments, bones and muscles, and is also essential for a healthy complexion due to its hydrating properties. Cucumbers are able to help lower blood pressure if consumed in sufficient quantities.


10- Asparagus
Aside from promoting healthy skin, asparagus also contains fiber and vitamin B6. It is a good food for pregnant women to consume due its high levels of folate, which also promotes heart health. Another advantage is that it is low in sodium, but contains potassium, and helps to maintain a healthy large intestine.


As outlined, it is difficult to put one vegetable ahead of another because of the similarities in nutritional content. Most would agree however that to improve or to maintain health, these vegetables should be consumed regularly as a part of a healthy diet.

SOURCE: www.methodsofhealing.com

Wednesday, January 27, 2010

BREAKING NEWZZZZ!!! OBAMA ALA KIAPO KUJENGA UPYA UCHUMI WA MAREKANI

Rais Barack Obama wa Marekani amekula kiapo cha kuijenga upya Marekani wakati wa hotuba take ya kwanza ya sikukuu ya Muungano.

Obama ameahidi kupatikana kwa ajira mpya zaidi ya milioni moja ikiwa ni sehemu ya ujenzi wa uchumi huo.


"Mabadiliko bado hayajaridhisha,” Alisema Obama. “Sikubaliani na nchi yangu kuwa katika nafasi hii.”

Rais Obama alirudia karibu mara tatu kauli yake hiyo ya kuujenga na upya uchumi wa hiyo, akisisitiza wazo la ukuaji wa ajira.



Mwaka mmoja baada ya dunia kukumbwa na mtikisiko wa uchumi lakini “bado hali hairidhishi,” Alisema.

R. KELLY KUCHIZISHA BOONGE LA CONCERT JUMAMOSI KAMPALA...

Robert Kelly anatarajia kufanya tonesho lake kuubwa katika Jiji la Kampala Uganda, Jumamosi hii.



Kwa wadau wa mambo haya kaeni chonjo tunakuja huko Kampala kuchizika pamoja... sawwaa!!!

HAWA NDIO WAUAJI WA MTOTO WA CHIFU FUNDIKIRA

Hatimaye washtakiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto wa chifu, Swetu Fundikira wamefikishwa mahakamani, Kisutu jijini hapa leo.


Sajini Rhoda Robert

Washtakiwa hao ambao ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Sajini Rhoda Robert na Koplo Ally Ngumbe wamesomwa mashtaka yao katika siku ya kwanza ya kesi yao mahakamani hapo leo.


Koplo Ally Ngumbe

MGAMBO WANAPOKOLEZA KIPIGO


Wakazi wa Dar es Salaam ambao ni wafanyakazi wa duka la Gulamali Sundries, Yakub Msanga (kulia) na Emmanuel Mbonde wakiwa na majeraha usoni baada ya kudaiwa kupokea kipigo kutoka kwa Mgambo wa Jiji (hawapo pichani) jana katika eneo lao la kazi baada ya kutokea kamatakamata eneo hilo lililopo Mtaa wa Kitumbini na Libya, Dar es Salaam jana. Wakazi hao wanadaiwa kutohusika na biashara za Kimachinga lakini waliambulia kipigo hicho wakati mgambo wakipita kukamata wamachinga

RAZA: MWACHENI KARUME

Mwansiasa na mfanyabiashara maarufu visiwani zanzibar, Mohammed Raza amesisitiza kuwa suala la Rais wa Zanzibar, Amani Karume kuongezewa muda ni la wazanzibari wenyewe na hivyo achwe.



Alisema hayo leo alipozungumza na wandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa hoteli ya starlight.

Tuesday, January 26, 2010

AFRIKA MASHARIKI KUTUMIA SARAFU MOJA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala amesema nchi za Afrika Mashariki zitaanza kutumia sarafu moja baada ya kuoitishwa kwa maazimio kadhaa katika Bunge la Afrika Mashariki.



Waziri Kamala alikuwa akitoa maelezo hayo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mkataba wa Huduma Bora kwa Mteja pamoja na Tovuti ya Wizara hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Jumuiya ya Afrika MAshariki leo jijini hapa Dar es Salaam.

TRA YAWAPIGA MSASA WA FORODHA NA USHURU WAFANYABIASHARA WAKUBWA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kitengo cha Forodha na Ushuru leo kimeendesha warsha ya siku moja ya Mafunzo kwa wafanyabiashara wakubwa juu ya Ushuru wa Forodha.



Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Mamlaka hiyo, Walid Juma amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa wafanyabiashara hao kuweza kuingia vema katika soko la pamoja la Afrika Mashariki pamoja na kuweza kupenya katika Soko la Kimataifa.

INDIA WASHEREHEKEA MIAKA 61 YA MUUNGANO

Raia wa Tanzania wenye asili ya India leo wamesherehekea Miaka 61 ya Muungano wa nchi yao katika Ofisi ya Ubalozi wa nchi hiyo iliyopo jijini hapa Dar es Salaam.



Balozi wa nchi hiyo Tanzania, Kocheril Bhagirath akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa nchi yake imeazimia kujenga miradi mikubwa hapa nchini ya Kielimu na Afya kwa lengo la kunufaisha watanzania.

Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Kituo Kikubwa cha Afya cha Kimataifa kitakachogharimu zaidi ya dola Milioni 20 za Marekani pamoja na Mradi mwingine wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambapo watanzania watapatiwa elimu ya Kompyut pamoja na Ajira.

Monday, January 25, 2010

UHUSIANO KATI YA BRAD PIT NA JENNIFER ANISTON UMERUDI?

Wasanii Brad Pitt na Jennifer Aniston wameonekana tena wakiwa pamoja.


Walionekana kwa pamoja jijini Los Angeles mwishoni mwa wiki katika harambee ya kusaidia waathirika wa Haiti.

VITA YA MAREKANI IRAQ HAIKUWA HALALI- WANASHERIA

Washauri waandamizi wa mambo ya sheria wa Serikali ya Marekani wakati wa vita ya Iraq dhidi ya Marekani wanatarajiwa kutoa maelezo yao baadaye kuwa wanaamini uvamizi wa kivita wa Marekani dhidi ya Iraq haukufuata sheria za Umoja wa Mataifa.



Maofisa hao watatoa ushahidi wao mbele ya Mwanasheria Mkuu mstaafu, Lord Goldsmith kesho (jumatano) pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Tony Blair siku ya Alhmaisi.

Mmoja wa Wanasheria hao, Sir. Michael Wood Mshauri Mkuu wa Mambo ya Sheria wa Mambo ya Nje atazungumzia uvamizi huo.

MAMIA KUMZIKA MTOTO WA CHIFU FUNDIKIRA KESHO MAKABURI YA MWANANYAMALA

Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanatarajia kumsindikiza aliyekuwa Mtoto wa Chifu Fundikira, Swetu Fundikira aliyeuawa kwa kudaiwa kupigwa na wanajeshi wa (jwtz), katika safari yake ya mwisho makaburi ya Mwananyamala kesho jijini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaka wa Mrehemu, Ismail Fundikira, marehemu anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Mwananyama saa tisa alasiri.


Marehemu Swetu enzi ya Uhai wake..

"Kwa sasa tunasubiri taratibu za 'postmortem' kumalizika pale Muhimbili National Hospital pamoja na kusubiri baadhi ya ndugu walio mbali kufika msibani." Alisema.

Hata hivyo Ismail amesema wao kama wanandugu wamejipanga kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya haki kutokana na uzito wa kesi yenyewe.

Marehemu Swetu ameacha Mke na watoto wawili Misuka na Syalo ambao wapo nchini Uingereza na Uholanzi
Marehemu Swetu alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi baada ya kushushiwa kipigo na Askari wawili wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) katika ugomvi wa barabarani, Mwananyamala, Dar es Salaam.


Marehemu Swetu na Mkewe enzi ya Uhai wake..

Hata hivyo wanajeshi hao walitiwa mbaroni na Jeshi la Polisi ambao wanashikiliwa katika kituo cha Salender Bridge.
Askari hao, ambao ni mtu na mkewe kutoka kambi ya Lugalo, wanadaiwa kumuua kijana huyo, Swetu Fundikira baada ya kumpiga wakiwa na mwanajeshi mwingine mmoja katika ugomvi wa barabarani uliotokana na askari hao kudai kuwa walifanyiwa fujo na kutukanwa na gari ambalo Swetu na wenzake walikuwa wamepanda.

Kwa mujibu wa taarifa za watu walioshuhudia tukio hilo na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Elias Kalinga zinasema marehemu alifariki juzi usiku katika Hospitali ya Muhimbili, kufuatia kipigo cha wanajeshi hao.

Habari kutoka kwa watu walioshuhudia tukio hilo zinasema kuwa askari hao walimpiga kijana huyo juzi katika eneo la Kinondoni A kwa madai kuwa aliwachomekea na gari lake.

"Askari hao walimshusha kwenye gari eneo la Kinondoni A na kuanza kumshushia kipigo. Baada ya kumpiga walimchukua na kumwingiza ndani ya gari lao na kuondoka naye," alisema mmoja wa mashuhudua hao, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Sunday, January 24, 2010

NDEGE KUBWA YA ABIRIA YATUMBUKIA BAHARINI

Ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Ethiopia, Boeing 737- 800 iliyokuwa imebeba abiria 92 na wafanyakazi imetumbukia baharini muda mfupi baada ya kuruka kutoka Beiruti kufuatia hali mbaya ya hewa.



"Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia yenye namba 409 imepata ajali muda mfupi baada ya kuruka majira ya saa 8.30 usiku ikiwa na abiria 83 wakiwemo wafanyakazi 9 wa ndege hiyo," Kwa mujibu wa taarifa ya ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Lebanon.

"Mashuhuda waliona mpira wa moto wakati ndege hiyo inatumbukia baharini," Aliendelea.

Ofisa huyo amesema kuwa waokoaji walijaribu kufika katika ndege hiyo kuona endapo watafanikiwa kukuta waliosalimika.

Thursday, January 21, 2010

ZAMBEZI AIRLINES WASHANGAA ABIRIA WA ZAMBIA

Shirika la Ndege la Zambezi limeelezea kitendo cha abiria wa Zambia wanaotumia usafiri wa mabasi badala ya Ndege za Shirika hilo pindi wanaporejea nchini kwao wakitokea Tanzania kuwa kinawapa ugumu katika biashara yao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya Fast Track Tanzania Ltd, ambao ni wakala wa Ndege hizo, Ofisa Mtendaji Mkuu, Don McDonald amesema kuwa abiria hao wanapokuja Tanzania kwa ajili ya kufanya shopping na kufanya shughuli nyingine kama za Kitalii, hutumia ndege zao lakini wanaporudi hutumia mabasi na hivyo kuwapa wakati mgumu katika biashara zao.


McDonald akielezea jambo kwa Wafanyakazi wa Fast Track Tanzania Ltd, na waandishi wa habari leo jijini hapa

KAWAMBWA, NAGU NA MKULO WAIBUKA BANDARINI

Dar es Salaam,
Mawaziri watatu wenye dhamana nyeti katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Shukuru Kawambwa wa Miundombinu, Dk. Mary Nagu wa Viwanda na Biashara na Mustafa Mkulo wa Fedha na Uchumi wamefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam inayomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kujionea utekelezaji wa shughuli zake leo jiji hapa.

Mawaziri hao walitembelea katika eneo lililokuwa likimilikiwa na NASACO ambalo kwa sasa lipo chini ya TPA na Kituo cha Kusafirishia Mafuta kujionea shughuli zinavyofanyika na mwisho kurejea katika chumba cha Mikutano kwa ajili ya kutoa Muhtasari kwa waandishi wa Habari.


Mawaziri, k. Shukuru Kawambwa wa Miundombinu na Dk. Mary Nagu wa Viwanda na Biashara wakiwa katika ziara hiyo leo

Wednesday, January 20, 2010

HUYU NDIYE MNET FACE OF AFRICA MTZ

TANZANIA’S Lilian Mduda has secured a slot for the Face of Africa finals planned for Lagos, Nigeria in February 6.

Lilian told reporters yesterday that she was proud to be among ten finalists for the grand finale whereas the winner for the model Search final will take home a 50, 000 Us dollar cash prize and a modelling contract with Oluchi‘s O Model Africa.

“I have trained well and every photo-shoot, every fashion fitting and every single time I get onto the catwalk, I live my dream because of Face of Africa” she said.
“I have come a long way from the Face of Africa Boot Camp which kicked off with 24 models from 16 countries - but after a tough week of challenges, tasks and no shortage of drama, only 10 made it for the finals and I am amongst” she said

Lilian, a University of Dar es Salaam Undergraduate student is expected to depart next Tuesday for South Africa where all the finalists would meet before heading for Nigeria.


Lilian Mduda

STANBIC YAPELEKA MMOJA ANGOLA 'CAN'

Benki ya Stanbic Makao Makuu, leo imekabidhi tiketi na fedha taslimu za kimarekani dola 1000 kwa Mshindi wa Shindano la 'Jiunge, Cheza na Ushinde' Bw. Severine Mtikile baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo, jijini hapa.

Bw. Mtikile atakwenda Luanda nchini Angola kushuhudia pambano la Robo Fainali litakalofanyika Jumapili ya wiki hii, akiwa na mwanaye Bryton. Benki hiyo itagharamia gharama zote kuanzia malazi na chakula mpaka hapo mshindi huyo atakaporejea nchini.


Washiriki wa warsha ya siku moja ya mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja

MAJAJI WAPIGWA MSASA


Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu na Makamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Warsha ya Mafunzo ya siku moja kuhusu Mkataba wa Nyongeza wa Umoja wa Mataifa wa Maputo protocol kuhusu Haki za Wanawake barani Afrika, iliyofanyika leo asubuhi Dar es Salaam.

Tuesday, January 19, 2010

WATANZANIA WASISITIZWA UMUHIMU WA KUJENGA VYOO NA KUVITUNZA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kutumia vyoo safi na salama ili kujikinga na magonjwa ya milipuko.

Mwakyusa alitoa rai hiyo wakati wa sherehe ya kuhitimisha Kampeni ya 'Fyatua Choo Ushinde' iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo asubuhi.

"Tujenge utamaduni wa kutumia vyoo safi na salama ili kuepuka magonjwa ya milipuko." Alisema

Kampeni hiyo iliyoanza mwanzoni mwa mwaka huu imehitimishwa leo ambapo washindi kadhaa walikabidhiwa zawadi zao.


Waziri Mwakyusa akiangalia baadhi ya picha za vyoo

Mjomba Mrisho Mpoto akishangilia jambo na wanafunzi wakati wa sherehe hizo

Monday, January 18, 2010

JK ASHTUKIA DILI, ACHOMOA KUKABIDHI GARI

Katika hali isiyotarajiwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliojitokeza kushuhudia tukio la makabidhiano ya magari mawili ya Wagonjwa 'Ambulance' Ikulu, Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete alikataa kukabidhi moja ya magari hayo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Kayange Jacob baada ya kubaini kuwa si mlengwa wa gari hilo.

Mambo yalikuwa hivi;
Mapema mnamo saa sita na nusu za mchana, wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliwasili Ikulu. Baada ya muda, Rais Kikwete naye aliwasili kwa ajili ya kukabidhi gari kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido (aliyemtarajia).

Waandishi wa habari walikuwa wamejipanga na kujiandaa na kamera zao tayari kwa kuchukua tukio hilo. Mkurugenzi yule naye ambaye hakuwa kusudio la Rais Kikwete naye alikuwa kajiandaa kwa kukabidhiwa gari lake.

Rais Kikwete alipokaribia eneo la tukio, akaanza kusalimia watu na kisha kuuliza, "We bwana unatokea wapi?, alimuuliza. "Natokea Ngorongoro mzee, " Alijibu. Rais Kikwete kama utani vile akazungumza, "Gari siyo yako bwana... Hii ni Kashfa kubwa, sikukabidhi gari bwana, gari hii wanatakiwa kukabidhiwa wanakijiji wa Engarinaibo na wala si Loliondo."

Baada ya hapo Rais Kikwete aliendelea kuhoji juu ya suala hilo, kisaha huyoooo akarudi zake ndani ya Ikulu na kuachwa maswali kibao kwa wandishi wa habari waliokuwepo pale pamoja na Mkurugenzi huyo naye asijue afanye nini baada ya kavukavu na Rais Kikwete.

Kwa hakika tukio hilo lilizua mijadala mikali kwa wandishi wa habari waliokuwepo eneo hilo mpaka wanaondoka.... Hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa ndugu msomaji.

Kwa uhondo zaidi tazama mfululizo wa tuki lenyewe katika picha hapo chini;


Magari yaliwasili katika viwanja vya Ikulu...


Punde Jk naye aliwasili tayari kwa kukabidhi


Baada ya hapo akamsalimia Mkurugenzi huyo na kuanza kumuhoji...


Baada ya kumuuliza mawili matatu akashangaa kulikoni...


Akazidi kusisitiza kuwa hakabidhiwi mtu gari hapa kama hahusiki...


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngorongoro kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka asijue la kufanya baada ya kupewa kavukavu za usoni na JK...

WIKI YA KIMATAIFA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU YAZINDULIWA DAR

Wiki ya Kimataifa ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu imezinduliwa leo Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa, Balozi Juma Bakari Mwapachu.

Akizindua wiki hiyo Balozi Mwapachu amewataka wafanyabiashara wakubwa, wafadhili mbalimbali kujitokeza kusaidia tukio hilo kwa lengo la kufanikisha azma hiyo.


Rais wa ISWiT Jokate Mwegelo akisistiza jambo..

Sunday, January 17, 2010

THE DREAM COME TRUE... SIMBA YAENDELEZA USHINDI



THE DREAM COME TRUE... Ndivyo usemavyo Ujumbe wa bango hili huku mshabiki wa klabu ya Simba akiwa na bendera yake juu ya bango hilo kusubiria kutimia kwa ndoto hiyo...

Ndoto ilitimia kweli baada ya Klabu hiyo kuichapa Majimaji kwa magoli 2-0 na hivyo kuendeleza rekodi yake ya ushindi wa kutokufungwa wala kutoa sare na timu yoyote inayoshiriki michuano hiyo.

Mechi hiyo ilifanyika jana katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salam ambapo Mshambuliaji hatari wa Simba, Mussa Hassan Mgosi aliipatia klabu yake hiyo magoli yote mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Thursday, January 14, 2010

Waliokufa kwa Mafuriko Haiti wafikia 50,000

Zaidi ya watu 50,000 wanahofiwa kufa katika tetemeko kubwa kuliko yote yaliyowahi kutokea katika Kisiwa cha Haiti, wakati timu ya uokoaji toka Uingereza ikiwa imeungana na waokoaji wengine.

Mamilioni ya watu wanahitaji msaada wa haraka ambao tayari umeanza kutolewa na nchi mbalimbali.

Rais Barack Obama wa Marekani aliahidi kuziomba nchi mbalimbali duniani kutoa misaada yote ya kibinadamu kusaidia wananchi wa Haiti kuondokana na Maafa hayo yaliyotokea.

Wakati huohuo zaidi ya wataalamu 70 wa uokoaji pamoja na Mbwa pamoja na zana hevi zimewasili katika Uwanja wa Ndege wa Gatwick usiku wa jana, zilizotolewa na Serikali ya Ulaya.


Eneo lililokumbwa na mfurio linavyoonekana kwa juu

waathirika wa mafuriko wakiwa katika eneo moja la hifadhi

HAKUNA WA KUNINYIMA USINGIZI JIMBONI- WASSIRA

Waziri wa Kilimo na Chakula, Steven Wassira amesema hata kama kuna wagombea ambao wamejitokeza kushindana nae katika Jimbo lake, hawamnyimi usingizi na kutamba kuwa atalitetea jimbo lake kutokana na kukubalika na wananchi.

"Unajua mwenye dhamana ya Jimbo ni mwananchi, hivyo yeye ndiye anayejua yupi wa kumpa kura yake kulingana na kipi alichokifanya jimboni humo,

"Hao waliojitokeza kushindana na mimi nawajua vizuri sana. Ndio walewale wa mwaka 2005 niliokuwa nashindana nao, hivyo hawaninyimi usingizi hata kidogo."

Wassira alikuwa akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake Dar es Salaam jana kuhusu hali ya Kilimo na Chakula iliyopo sasa kutokana na mvua zilzioanza kunyesha.

Wednesday, January 13, 2010

TBL YAMWAGA JEZI SIMBA NA YANGA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU


Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja (kulia) akikabidhi jezi kwa Mwakilishi wa Simba, Mohamed Mjenga (kushoto) ikiwa ni moja ya vifaa vilivyotolewa na Bia ya Kilimanjaro kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Utawala na Uanachama TFF, Mtemi Ramadhani.

MAREKANI YAMTUNUKU JK TUZO YA MALARIA


Rais Jakaya Kikwete akipokea tuzo maalum ya ubingwa katika mapambano dhidi ya malaria kutoka kwa Mwenyekiti wa Malaria Center ya Marekani, Peter Chernin, wakati Mwenyekiti huyo alipomtembelea Ikulu Dar es Salaam jana

Tuesday, January 12, 2010

BREAKING NEWZZZZZZZZ: MAMIA WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA TETEMEKO HAITI

Mamia ya watu wamehofiwa kufa kufuatia tetemeko kubwa lililotokea Haiti. Haiti ni moja ya Kisiwa cha Carribean.
Majengo makubwa yakiwamo Hospitali, Hoteli, Jengo la Benki ya Dunia pamoja na Makazi ya Rais yaliharibiwa vibaya na tetemeko hilo ambalo halijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 200.

Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wanahofia kuwa mamia ya watu hata kufikia maelfu juenda wakawa wamepoteza maisha katika tetemeko hilo lililotokea katika kipimo cha Richa 7.1

Ilichukua takribani saa moja kwa tetemeko hilo kuharibu vibaya eneo kubwa la mji wa Port-au-Prince, uliopo maili 10 kutoka mji mkuu wa Kisiwa hicho


Wakazi wa Haiti wakikimbia baada ya tetemeko hilo

Moja ya gari likiwa limefunikwa na kifusi baada ya tetemeko hilo

SOURCE: SKY NEWS

WANATAALUMA WAZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA KUCHANGIA WAHANGA WA MAFURIKO

Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN) kwa kushirikiana na Mitandao ya www.jamiiforums.com, www.issamichuzi.blogspot.com na Mtandao wa Habari, Burudani na Harakati za Kisiasa wa www.mwanakijiji.com na Push Mobile umezindua Kampeni ya Kusaidia wahanga wa Mafuriko yaliyoikumba meneo mbalimbali ya nchi hapa jijini.

Kwa wale watakaopenda kutoa michango yao kupitia TPN watoe kwa njia zifuatazo:

1. Crossed Cheque, written to: Tanzania Professional Network
2. Bank Deposits or Transfers to: Account Name: Tanzania Professionals Network, Bank Name: CRDB Bank, Bakn Branch: Lumumba Branch, City: Dar es Salaam, Country: Tanzania, Swift Code: CORUTZ TZ, US $ A/C No: 02J1 007 608 900: TZS A/C No: 01J1 007 608 901
2. M-PESA (Vodacom): 0768 777 888
4. Z-Pesa (Zantel): 0773 88 18 88
5. Zaap (Zain) 0784 00 88 99
6. Western Union- Tuma kwa: Mr. Emmanuel Mmari: TPN Finance and Administrative Manager; Dar es Salaam. Tuma Nakala ya MTCN kwa president@tpn.co.tz
7. Fedha Taslimu: Ofisi za TPN- Barabara ya Nyerere: Jengo la TOHS (Dar Group); Ghorofa ya 1, karibu na Radio Tanzania.
8. Kuchangia kupitia makato ya kila siku ya muda wa maongezi: Changia shs 150 kwa siku kwa waathirika wa mafuriko. Tuma sms yenye neno TPN kwenda 15522. Utakatwa shs 250 kujisalili. Kwa Maelezo zaidi wasiliana na 0715 740 047


Mkurugenzi wa Jamii Media inayomiliki tovuti ya Jamii Forum, Maxence Melo (kushoto) akisistiza jambo wakati wa Mkutano na waandishi kuhusu Kampeni hiyo leo Dar es Salaam. Mwingine ni Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), Sanctus Mtsimbe

Monday, January 11, 2010

Wawili wanaswa kufuatia shambulio dhidi ya Togo

Watu wawili wamekamatwa wakihusishwa na Shmabulio dhidi ya Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Togo, Kituo cha Habari cha Angola kimeripoti

Katika shambulio hilo watu wawili walikufa baada ya kushambuliwa kwa risasi katika basi walilokuwa wamepanda kuelekea Angola, katika Mji wa Cabinda, Ijumaa iliyopita.

Watu hao waliokamatwa wakihusishwa na shambulio hilo walikutwa eneo la jirani na shambulio lilipotokea, kwa mujibu wa Radio hiyo.


"Watu wawili wamenaswa. Tutakapokuwa na taarifa kamili tutaitoa kwa wananchi." Mwansheria Mkuu wa jimbo la Cabinda, Angola, Antonio Nito alikiambia kiyuo hicho.

Katika shambulio hilo, Kocha Mkuu Msaidizi wa timu hiyo, Amalete Abalo pamoja na Msemaji wa timu hiyo, Stanislas Ocloo walikufa pamoja na dereva wa basi lililobeba wachezaji ambapo wengine nane walijeruhiwa.

Kikosi hicho sasa kimerejea nyumbani Togo. Wachezaji walitaka kubaki kucheza kwa ajili ya kuomboleza wenzao waliokufa, lakini Serikali ya nchi hiyo ilitoa amri ya kurudi nyumbani kwa timu hiyo.
SOURCE: SKY NEWS


Nahodha wa Timu ya Taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor