Monday, January 11, 2010

Wawili wanaswa kufuatia shambulio dhidi ya Togo

Watu wawili wamekamatwa wakihusishwa na Shmabulio dhidi ya Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Togo, Kituo cha Habari cha Angola kimeripoti

Katika shambulio hilo watu wawili walikufa baada ya kushambuliwa kwa risasi katika basi walilokuwa wamepanda kuelekea Angola, katika Mji wa Cabinda, Ijumaa iliyopita.

Watu hao waliokamatwa wakihusishwa na shambulio hilo walikutwa eneo la jirani na shambulio lilipotokea, kwa mujibu wa Radio hiyo.


"Watu wawili wamenaswa. Tutakapokuwa na taarifa kamili tutaitoa kwa wananchi." Mwansheria Mkuu wa jimbo la Cabinda, Angola, Antonio Nito alikiambia kiyuo hicho.

Katika shambulio hilo, Kocha Mkuu Msaidizi wa timu hiyo, Amalete Abalo pamoja na Msemaji wa timu hiyo, Stanislas Ocloo walikufa pamoja na dereva wa basi lililobeba wachezaji ambapo wengine nane walijeruhiwa.

Kikosi hicho sasa kimerejea nyumbani Togo. Wachezaji walitaka kubaki kucheza kwa ajili ya kuomboleza wenzao waliokufa, lakini Serikali ya nchi hiyo ilitoa amri ya kurudi nyumbani kwa timu hiyo.
SOURCE: SKY NEWS


Nahodha wa Timu ya Taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor

No comments:

Post a Comment