Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman kova leo amewasihi wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutopenda kujihusisha na vurugu ambazo mwisho wake hupelekea jeshi lake kutumia nguvu za dola sheria dhidi yao.
Kamishna Kova amesema kuwa kwa mujibu wa desturi za kiafrika, unapompiga mzee huenda ukapata lana kutoka kwa mungu na hivyo si jambo jema kwake kuwachukulia hatua za kipolisi ambazo mwisho wake huwa ni maumivu.
'Mimi naogopa laana wazee wangu. Sipendi mimi kuona mnachukuliwa nguvu za kisheria dhidi yenu." Aliwasihi na kuendelea, "Kwa wale wanaoamini kitabu cha Qur'an kinasema kuwa Innallaah maa swaabirina... Maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu yupo karibu na mwenye subira.. hivyo bawasihi mfanye subira hili jambo lenu nitalishughulikia mimi pamoja na hawa viongozi wenu", Alimaliziia kwa kusema hivyo na kuwafanya wazee hao waliokuwa wamekusanyika mbele ya Kituo Kikuu cha Polisi 'Central Police' kumshangilia kwa makofi...
Kisha akawasihi wazee hao kwa kuwaambia tena, "Hivyo nawaomba wazee wangu muende nyumbani kwa amani... hili suala niachieni mimi na viongozi wenu mliowaamini... sawa jamani?" Alimalizia kwa kusema hivyo na kisha wazee wale baada ya sekunde chache wakaridhia maneno yake na wakaondoka zao...
Wazee wa Afrika Mashariki wakiondoka zao baada ya kumwagiwa aya na Kova...
No comments:
Post a Comment