Monday, June 1, 2009

Mechi Taifa Stars na New Zealand: 'Watakavunja amani kukiona' - KOVA

KAMANDA wa Polisi Kikosi Maalumu, Dar es Salaam, Suleiman Kova amewahakikishia watanzania hususan washabiki wa mpira watakaokwenda kuangalia pambano la kimataifa la kirafiki kati ya Taifa Stars na timu ya New Zealand, kuwepo kwa usalama wa kutosha kutokana na Jeshi lake kujipanga vilivyo katika ulinzi.

Kamanda Kova amesema kuwa Jeshi lake litatumia mbinu na njia za kisasa za kiteknolojia ya hali ya juu kuhakikisha vitendo vyovyote vya kihalifu na uvunjaji amani vinazimwa kabla ya kufanyika. Njia hizo ni pamoja na ufungaji wa camera za cctv ambazo zitakuwa zikinasa matukio yote ya uvunjaji wa amani wakati wa mpambano huo, uwanjani hapo.

"Ile 'big screen' ya uwanjani itakuwa ikionyeha live matukio yote ya uvunjaji amani yatakayokuwa yanatendeka. Na muhalifu akikamatwa hakuna cha 'msalie mtume.'' Alisema Kova.

Aidha Kamanda Kova amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi ili kuishangilia timu hiyo ya Taifa Stars ili kuipa nguvu. "SIku hiyo Baba, Mama na watoto wataweza kuja kushuhudia mechi hiyo na watakaa kwa amani na kuondoka kwa amani kutokana na ulinzi utakaokuwepo hapo. Hakutatokea vitendo vyovyote vya uvunjaji amani, wahalifu watashughulikiwa ipasavyo, tumejipanga vilivyo." Alisema Kova.

Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki kati ya Taifa Stars na New Zealand inatarajiwa kufanyika jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, jijini hapa.


Kamanda Kova akifafanua jambo kwa wanahabari, leo jijini...

No comments:

Post a Comment