Treni ya mizigo ambayo ni Mali ya TAZARA iliyokuwa ikitokea bandari ya nchi kavu na kuelekea Bandarini imegonga daladala katika makutano ya Barabara ya Buza na Reli ya Tazara, eneo la Yombo Davis Corner ambapo watu 27 wamejeruhiwa na mmoja kufa papohapo leo majira ya saa tano asubiuhi.
Shuhuda wa ajali hiyo wameiambia Blogu hii ya Sponsor kuwa awali dereva wa dalada hilo linalofanya safari zake kati ya Tandika na Buza, alishindwa kulimudu gari lake baada ya kuzimika katikati ya Reli wakati treni hiyo ya Mizigo ilipokuwa inapita na hivyo kusababisha ajali ambapo gari hilo liligongwa na kuzunguka zaidi ya mara mbili kabla ya kutupwa pembezoni mwa reli.
"Daladala lile lilikuwa likitokea Tandika kuelekea Buza, treni ilipiga honi mara Moja lakini dereva wa daladala sifahamu kwa nini aliamua kupita pale." Alisema Mmoja wa Mashuhuda.
Sponsor ilipiga mwendo mpaka Kituo cha Polisi cha Chang'ombe ambapo daladala hilo lenye namba za Usajili T ALX lilikuwa limehifadhiwa pale na kulikuta likiwa limegongwa zaidi katika Upande wa kulia ambao ndio upande wa dereva.
Baadaye Sponsor ilielekea katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke ambapo Majeruhi walikuwa wamefikishwa phapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambo wengi wao walikuwa wakiendelea kupatiwa matibabu ikiwemo ni pamoja na kushonwa maeneo mbalimbali waliyokuwa wamechanika.
PICHA MBALIMBALI ZA AJALI.
No comments:
Post a Comment