Nakukaribisha katika Blogu ya Akida uhabarike kwa habari za Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani zilizotokea na zitakazotokea... 'be the First to know..!
Monday, March 22, 2010
MVUA, WATOTO NA HATARI BARABARANI
Nimegundua kuwa watoto wenye umri mdogo hasa wale walio darasa la kwanza, hupenda kucheza katika mvua pindi zinaponyesha.
Katika pitapita zangu za kutafuta habari leo asubuhi nikianzia wilayani Kinondoni, Ilala na kumalizia Temeke nimekutana na watoto ambao ni wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya hizo wakiwa vifua wazi huku wakikimbizana katikati ya mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha kwa mafungu jijini hapa.
Nilipigwa butwaa nilipowaona watoto wakikatiza barabara ya Kawawa eneo la Kigogo, wakikimbia pasipo kuangalia usalama wao huku magari yaendayo kasi yakipishana nao.
Hali hiyo ilinistaajabisha na kutafakari kuhusu umuhimu wa wazazi kuchukua tahadhari kwa watoto wao pindi mvua zinaponyesha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment