Monday, February 8, 2010

AJALI YA TRENI YAJERUHI 27 NA KUUA 1 DAR

Treni ya mizigo ambayo ni Mali ya TAZARA iliyokuwa ikitokea bandari ya nchi kavu na kuelekea Bandarini imegonga daladala katika makutano ya Barabara ya Buza na Reli ya Tazara, eneo la Yombo Davis Corner ambapo watu 27 wamejeruhiwa na mmoja kufa papohapo leo majira ya saa tano asubiuhi.

Shuhuda wa ajali hiyo wameiambia Blogu hii ya Sponsor kuwa awali dereva wa dalada hilo linalofanya safari zake kati ya Tandika na Buza, alishindwa kulimudu gari lake baada ya kuzimika katikati ya Reli wakati treni hiyo ya Mizigo ilipokuwa inapita na hivyo kusababisha ajali ambapo gari hilo liligongwa na kuzunguka zaidi ya mara mbili kabla ya kutupwa pembezoni mwa reli.

"Daladala lile lilikuwa likitokea Tandika kuelekea Buza, treni ilipiga honi mara Moja lakini dereva wa daladala sifahamu kwa nini aliamua kupita pale." Alisema Mmoja wa Mashuhuda.


Sponsor ilipiga mwendo mpaka Kituo cha Polisi cha Chang'ombe ambapo daladala hilo lenye namba za Usajili T ALX lilikuwa limehifadhiwa pale na kulikuta likiwa limegongwa zaidi katika Upande wa kulia ambao ndio upande wa dereva.

Baadaye Sponsor ilielekea katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke ambapo Majeruhi walikuwa wamefikishwa phapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambo wengi wao walikuwa wakiendelea kupatiwa matibabu ikiwemo ni pamoja na kushonwa maeneo mbalimbali waliyokuwa wamechanika.

PICHA MBALIMBALI ZA AJALI.







Thursday, February 4, 2010

LAW DAY CELEBRATIONS IN PICTURES

Picha zote:
Rais Jakaya Kikwete, Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan na Spika wa Bunge la Tanzania, Samwel Sitta wakiwa katika maadhimisho hayo.




JK ATAKA MAHAKAMA KUHARAKISHA UTOAJI HUKUMU

Rais Jakaya Kikwete amezitaka Mahakama nchini kurekebisha kasoro zinazolalamikiwa na wananchi ambazo zinatia doa mwenendo wa utoaji haki nchini.

Rais Kikwete alisema hayo wakati akihutubia jopo la Majaji wakuu wa Mahakama, Mawakili na Wanasheria wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo asubuhi katika eneo la Mahakama Kuu, jijini hapa.

"Bado kuna malalamiko kuhusu ucheleweshaji wa usikilizaji kesi na utoaji hukumu pia. Aidha, kuna malalamiko kuhusu kuchelewa kuandikwa kwa hukumu na kuna kilio cha baadhi ya watumishi wa mahakama kuomba na kupokea rushwa," Alisema na kuendelea,

"Kasoro hizo zinatia doa katika mwenendo mzima wa utoaji haki nchini. Hamna budi kufanya kila iwezekanavyo kuziondoa kasoro hizo. Naamini inawezekana. Naamini mnaweza. Yes you can," Akaendelea tena,

"Nafurahi kwamba wenyewe mnatambua hizo kasoro na mnachukua hatua kuzirekebisha." Alisema Rais Kikwete.



Hata hivyo Rais Kikwete amewasifu Majaji wa Mahakama ya Rufani kwa kitendo alichokiita cha Kizalendo zaidi cha kuacha kwenda kula Sikukuu za mwisho wa mwaka jana, badala yake kufanya Kikao kwa ajili ya kumalizia mashauri takribani 82 ambayo hata hivyo ni Mashauri 61 kati ya hayo ambayo yamesikilizwa na yanayosuburi kutolewa Maamuzi ni 8.

"Nimefurahishwa sana na kitendo cha kizalendo, niliposikia kwamba Majaji wa Mahakama ya Rufani, waliacha kwenda kwenye mapumziko ya “Chrismas Vacation” ya mwaka jana, mapumziko ambayo hufanyika kila mwezi wa Disemba mpaka Januari, badala yake wamekaa na kufanya kikao maalum (special session) ambacho kimemalizika tarehe 29/01/2010" Alisema.

Wednesday, February 3, 2010

JK MGENI RASMI KONGAMANO KUBWA LA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano kubwa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano linalotarajiwa kufanyika tarehe 8 na 9 ya mwezi Machi mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond.



Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa Kongamano hilo jijini Dar es Salaam leo, Rais wa Jopo la Wataalamu Afrika Mashariki, Paul Mashauri amesema hiyo ni fursa ya pekee kwa watanzania kujifunza na kuzifahamu changamoto mbalimbali zinazokabili sekta hiyo nchini.

BINGO MPYA KUANZISHWA

Kampuni ya Entertainment afica ltd, leo imekabidhiwa rasmi leseni ya uendeshaji wa biashara ya michezo ya kubahatisha ya Bingo.

Katika michezo ambayo Kampuni hii itakuwa ikiichezesha ni pamoja na Easy Bingo ambao ni mchezo mpya wa kubashiri namba.

Premier Bingo ni Mchezo wa kila siku unaochezeshwa kwenye kadi maalumu zinazopatikana kwa mawakala walioidhinishwa na kampuni hiyo. Kwa kawaida hizi huuzwa kwa bei ya sh 1000.


Abbas Tarimba akikabidhi cheti kwa Meneja Uendeshaji wa Kampuni hiyo