Monday, May 24, 2010

JK AWAPASHA MAOFISA WA DAWASA, EWURA LIVE

Rais Jakaya Kikwete kama ilivyo kawaida yake ya kuwatolea uvivu watendaji wasiowajibika kwa wananchi wao, leo amewapasha maofisa wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini (DAWASA) na wale wa Mamlaka inayodhibiti Maji na Nishati (EWURA) 'live' bila chenga kwa kuwaambia waache ubabaishaji na blablaa badala yake wawe watendaji zaidi.

'JK' aliwapasha maofisa hao mbele ya 'wapiga kura' wake katika maeneo tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti alipofanya ziara katika maeneo hayo kuangalia maendeleo ya upatikanaji wa Majisafi kwa wananchi hao ikiwa ni ziara yake maalumu jijini hapa.

"Hawa ndiyo wanaowalalimikieni na si mimi. Wasikilizeni wanataka nini na muwatimizie, vinginevyo hawatawaelewa hawa!!" Aliwaambia maofisa hao na kuongeza, "Watekelezeeni mahitaji yao na muwache blaa blaa..." Alisema huku akishangiliwa na mamia ya wananchi hao waliofurika katika maeneo hayo tofautitofauti.

PICHA ZAIDI

Rais Kikwete akihutubia



Sehemu ya wananchi waliofurika kumshuhudia Rais Kikwete

Rais Kikwete akiongea na watoto wa chekechekea ya Gift ya Keko

Sunday, May 23, 2010

TWIGA STARS MPANGO MZIMA! YAICHAPA ERITREA 8-1

Timu ya Taifa ya wanawake 'Twiga Stars' leo imefanikiwa kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake baada ya kuinyuka Eritrea kwa jumla ya magoli 8-1.

Mwanahamisi Omary na Asha Rashidi waling'ara uwanjani baada ya kila mmoja kuondoka na kapu la magoli ya kutosha, ambapo Mwanahamisi aliondoka na magoli manne huku Asha akiondoka na magoli 3.

Kwa matokeo hayo, Twiga Stars itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya timu hiyo Eritrea mjini Asmara.


Wachezaji wa Twiga Stars wakishangilia baada ya kumalizika kwa mchezo

Mwanahamisi Omary 'Redondo' (juu) akiruka kihunzi cha beki wa Eritrea, Semhar Bereket Bhabla

PICHA ZAIDI

Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Dar Inter-College wakiwa katika picha ya pamoja na kipa no.1 Fatuma Omary

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika akizungumza na wandishi wa habari baada ya pambano

Makipa wa Twiga (kulia na Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo

Kipa namba 1 Fatuma Omary akiwa katika picha ya pamoja na warembo

Thursday, May 20, 2010

MWANANYAMALA HOSPITALI DOLE TUPU- LUKUVI

Mkuu wa Mkoa huu leo amefanya ziara katika hospitali ya Mwananyamala na kusema kwamba ni safi kuliko watu wanavyodhania.

"Ukiwa nje watu wanaizungumzia vibaya, lakini leo nimekuja mwenyewe nimejionea. Mna mshikamano na mnafanya kazi kwa moyo mmoja." Alisema.

Hii si kawaida hata mara moja kwa viongozi wa ngazi za juu Serikalini kufanya ziara hospitalini hapo na kumwaga sifa kemkem kama ilivyo leo kwa Lukuvi.


Lukuvi akipita katikati ya wazazi waliopo wodini