Monday, June 15, 2009

Magereza Ukonga kuanzisha Hifadhi ya Wanyama

Nilipokaribia eneo hilo ambalo ni kambi ya Magereza ya Ukonga, nilistaajabu kuona misitu ya asili iliyoshibana na kupelekea hewa safi kuzunguka eneo. Baada ya kushuka garini Mkuu wa Kikosi Maalumu cha Magereza, Menrad Tesha alitutembeza kuangalia baadhi ya vivutio vya asili vilivyomo katika eneo hilo.

"Kwa ujumla eneo lote la hifadhi lina ukubwa wa ekari 1000." Alianza kwa kusema ACP Tesha na kuendelea, "Eneo hili linapakana na hifadhi ya wanyama ya Selous, upande wa Kusini Mashariki pamoja na Kijiji cha Kiboga." Alisema.

Baadaye tukafika eneo ambalo kuna msitu pamoja na kuweka vichaka vilivyofungamana ambalo kwa mujibu wa Kamanda Tesha alisema ni makazi ya Tembo. "Si tembo tu, wakati mwingine unaweza kuwaona Simba, Duma, Swala na Chui." Alisema. Nilishangazwa zaidi tulipofika katika bwawa la matope la kuhifadhi viboko. Duh, nilistaajabu kweli haki ya Mungu.

bwawa hilo ambalo juu yake kumestawi majani ama magugu yanayohifadhi maji ni kubwa kweli ambalo unaweza kulilinganisha na lile la Mindu kule Morogoro. Nilijaribu kudodosa kidogo kutaka kufahamu historia ya hilo bwawa, nikaambiwa kuwa hapo awali kulikuwa na kijiji fulani hivi kabla ya kuzama na kutengeneza bwawa hilo.

Baadaye tulipomaliza kuzungukia maeneo hayo mbalimbali, tukajipumzisha mahali kupata madafu na machungwa. Kwa kweli nilivutiwa sana na eneo hilo kwa ujumla. Nikagundua kuwa, unaweza kufanya utalii wa kutosha eneo hilo badala ya kwenda mbali na nje ya jiji hili.

Hiyo ndiyo Hifadhi ya Kambi ya Magereza ya Ukonga, iliyopo eneo la Mvuti, wilayani Ilala jijini hapa ambayo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali tulifanya ziara kuangalia vivutio vya kitalii mwishoni mwa wiki iliyopita.


waandishi wa habari wakipenya katika moja ya miti iliyofungana katika hifadhi hiyo..


waandishi wa habari wakipenya katika moja ya vichaka vya hifadhi hiyo..


Moja ya kisima chenye historia kubwa ya hifadhi hiyo...


ACP Menrad Tesha (kushoto) akiwaongoza baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa Magereza kuangalia bwawa la matope linalohifadhi viboko hifadhini hapo...

Monday, June 8, 2009

Kuagwa kwa Marehemu Beatha katika Picha...


Wanafunzi wa DUCE wakiamuaga mwenzao, marehemu Beatha...

Sanduku lililobeba mwili wa marehemu Beatha likiwasili chuoni DUCE kwa kuagwa.. Matukio yote ni leo mchana

Mwanafunzi aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na mpenziwe aagwa


Marehemu Beatha Mwarabu, mwanafunzi wa DUCE aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na mpenzi wake akiwa na tabasamu kabla ya kifo chake...

Friday, June 5, 2009

SAUT Tawi la Dar yazinduliwa rasmi

Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Tawi la Dar es Salaam kimezinduliwa rasmi leo na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, jimbo kuu la Dar es Salaam, Muhashamu Kadinali Pengo.

Chuo hicho kinachotoa shahad ya uzamili pamoja na udaktari katika masomo ya Mawasiliano ya Jamii, kitakuwa ni cha kwanza kutoa vyeti vya ngazi hiyo kwa Tanzania.


Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muhashamu Kadinali Pengo akibariki baadhi ya madarasa ya chuo cha SAUT, tawi la Dar es Salaam mara baada ya kukizindua rasmi leo mchana...

Tuesday, June 2, 2009

SIMU ZA SOLAR KUINGIA NCHINI

Ni za COMMTIVA... Simu hizi hazitumii umeme, zinajichaji kwa mwanga wa jua... wakazi wa maeneo ya vijijini wanatarajia kunufaika zaidi...

Monday, June 1, 2009

Miss mzizima kuzizima Jumamosi wiki hii


Baadhi ya warembo watakaoshiriki shindano la 'Miss Mzizima', Dar es Salaam wakiwa katika pozi walipotembelea makao makuu ya Vodacom, leo asubuhi...

Liyumba kuendelea kusota Mahabusu

Mtuhumiwa wa kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali ya zaidi ya bilioni 200, Amatus Liyumba amerudishwa tena mahabusu baada ya dhamana yake kugonga mwamba kutokana na kushindwa kutimiza masharti yake mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Ngigulila Mwaseba.

Liyumba na mawakili wake waliwasilisha vivuli vya hati ya mali ambavyo mahakama ilitupilia mbali ombi hilo, na kuhitaji hati halisi, na hivyo Hakimu kuamuru Liyumba kurudishwa mahabusu mpaka tarehe 15 ya mwezi juni kwa ajili ya kusikiliza tena maombi hayo ya dhamana.

SOURCE: Neema Mgonja


Liyumba (kushoto) akiteta jambo na wakili wake, Majura Magafu...

Mechi Taifa Stars na New Zealand: 'Watakavunja amani kukiona' - KOVA

KAMANDA wa Polisi Kikosi Maalumu, Dar es Salaam, Suleiman Kova amewahakikishia watanzania hususan washabiki wa mpira watakaokwenda kuangalia pambano la kimataifa la kirafiki kati ya Taifa Stars na timu ya New Zealand, kuwepo kwa usalama wa kutosha kutokana na Jeshi lake kujipanga vilivyo katika ulinzi.

Kamanda Kova amesema kuwa Jeshi lake litatumia mbinu na njia za kisasa za kiteknolojia ya hali ya juu kuhakikisha vitendo vyovyote vya kihalifu na uvunjaji amani vinazimwa kabla ya kufanyika. Njia hizo ni pamoja na ufungaji wa camera za cctv ambazo zitakuwa zikinasa matukio yote ya uvunjaji wa amani wakati wa mpambano huo, uwanjani hapo.

"Ile 'big screen' ya uwanjani itakuwa ikionyeha live matukio yote ya uvunjaji amani yatakayokuwa yanatendeka. Na muhalifu akikamatwa hakuna cha 'msalie mtume.'' Alisema Kova.

Aidha Kamanda Kova amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi ili kuishangilia timu hiyo ya Taifa Stars ili kuipa nguvu. "SIku hiyo Baba, Mama na watoto wataweza kuja kushuhudia mechi hiyo na watakaa kwa amani na kuondoka kwa amani kutokana na ulinzi utakaokuwepo hapo. Hakutatokea vitendo vyovyote vya uvunjaji amani, wahalifu watashughulikiwa ipasavyo, tumejipanga vilivyo." Alisema Kova.

Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki kati ya Taifa Stars na New Zealand inatarajiwa kufanyika jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, jijini hapa.


Kamanda Kova akifafanua jambo kwa wanahabari, leo jijini...

Kampuni ya ukopeshaji fedha yazinduliwa

Kampuni ya kifedha ya GroFin Tanzania imezinduliwa leo asubuhi na kutoa fursa kwa wananchi kwenda kukopa fedha kwa ajili ya kuendeshea biashara na miradi yao mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa GroFoin- Tanzania, Ezra Musoke amewataka wananchi kwenda kwa wingi kukopa fedha katika Kampuni hiyo ambapo amesema mikopo yao ni nafuu ambayo wananchi wengi wanaweza kumudu.


Ofisa Mkuu wa Uwekezaji wa GroFin Africa, Guido Boysen akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari leo...

Waathirika wa mabomu waomba kuhamishwa

Wakazi wa Mbagala, waathirika wa milipuko ya mabomu wameitaka Serikali kuwahamisha eneo hilo kwa madai kuwa usalama wa maisha yao upo hatarini.

Mmoja wa wakazi hao, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Jacky amesema kuwa tangu walipoanza kuishi maisha ya kambini, afya zao pamoja na za watoto zimekuwa zikiathirika siku hadi siku kutokana na mazingira yaliyopo eneo hilo.

Amesema kuwa, wakati mwingine wanalazimika kuyahama makazi yao kwa muda inapotokea taarifa kuhusu kulipuliwa kwa mabomu mengine, jambo linalowafanya kuishi maisha ya wasiwasi.

"Zamani Kilungule nilikuwa napaona mbali sana ukilinganisha na siku hizi ambapo napaona ni karibu hasa kunapokuja taarifa za kulipuliwa kwa mabomu. Huwa nakimbia mpaka huko." Alisema Mama Jacky.


Mkazi wa Mbagala akionyesha nyumba yake ilivyoteketezwa kwa mabomu...