Thursday, July 16, 2009

Uchafu Kariakoo mwendo mdundo...

Siku chache baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuripoti habari za kuondolewa kwa taka zilizokuwa zimerundikana katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, blog hii imeshuhudia kurejea kwa taka hizo kwa kasi katika makutano ya mtaa wa Congo na Aggrey leo mchana.

Wafanyabiashara pamoja na wakazi wa jiji hili walionekana kuendelea na shughuli zao kwa tabu juu ya mrundikano wa taka hizo ambazo zilikuwa zikitoa harufu kali na kusababisha kero kwa wapita njia.


Mkazi wa jijini akijaribu kupunguza taka zilizokuwa zimerundikana eneo hilo na kuwa usumbufu kwa wafanyabiashara na wapita njia

No comments:

Post a Comment