Monday, July 20, 2009

Wanafunzi Kairuki wagomea ongezeko la ada

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert KAiruki wamegomea ongezeko la asilimia 25 ya ada lililowekwa na uongozi wa chuo hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa Serikali ya wanafunzi hao wamesema kuwa ongezeko hilo linawanyima haki ya kupata elimu kutokana na uwezo wao kifedha pamoja na wanaowafadhili kuwa ni mdogo.

Pia wamesema si jambo la kiungwana kwa uongozi huo kusubiri bajeti ya seikali ya mwaka huu 2009/2010 kupitishwa ndipo waongeze kiwango hicho cha ada kwani wafadhili wao ikiwamo Serikali watashindwa kumudu gharama hizo.


Baadhi ya wanafunzi hao wakiwa nje ya majengo ya chuoni kwao wakijadili ongezeko hilo la ada...

No comments:

Post a Comment