Nakukaribisha katika Blogu ya Akida uhabarike kwa habari za Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani zilizotokea na zitakazotokea... 'be the First to know..!
Wednesday, April 8, 2009
DECI wakomaa kinoma
Katika hali ya kushangaza na kuonyesha kukomaa kihuduma zaidi, Jumuiya ya Maendeleo ya Wajasiriamali (DECI), wameikomalia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuwa kamwe hawapo tayari kuona inaifungia jumuiya hiyo kuendelea na huduma zake.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara na wanachama wa Jumuiya hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya DECI, Askofu Bartholomew Sheggah amesema kuwa jumuiya yake haiwezi kuacha kuendelea kutoa huduma ya kuwasaidia wananchi walo na hali ya chini kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamekiuka malengo ya Rais Jakaya Kikwete ya 'Maisha bora kwa Kila Mtanzania'
"Wanaotaka Jumuiya yetu ifungiwe hao wana nia mbaya na hawataki wananchi wajikwamue katika hali ngumu ya maisha. Sisi tunatimiza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya 'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania'." Alisema.
Mkutano huo uliofurika maelfu ya wanachama hao ulikuwa na lengo la kutolea ufafanuzi wa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuhusu kusimamishwa kwa jumuiya hiyo kutokana na madai kuwa haitambuliki kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment