Sunday, April 26, 2009

Mrema awazuia Mutungirehi na Kinanda kuingia Mkutanoni

Katika hali inayooonyesha demokrasia kwa baadhi ya vyama vya siasa nchini kutokukomaa, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Lyatonga Mrema amewatimu wagombea wa nafasi za uongozi wa juu katika chama hicho katika mkutanoni mkuu wa taifa wa uchaguzi wa chama hicho, Joram Kinanda na Mutungirehi leo jijini hapa.

Wakiwa wamesimama nje ya ukumbi wa mkutano huo wagombea hao wameiambia Sponsor kuwa awali walipewa mwaliko wa kuhudhuria Mkutano huo na Mwenyekiti wao, Mrema lakini wameshangaa hatua ya kuzuiwa kuingia mkutanoni muda mfupi baada ya kuwasili.

Kwa upande wake, Mrema amesema kuwa wagombea hao wamevamia mkutano huo pasipo kualikwa jambo lililopelekea kuwazuia wasiingie mkutanoni kwa kuhofia wangeleta vurugu kubwa kutokana na tofauti zilizopo baina ya wagombea hao na Mrema.

Mkutano Mkuu wa Taifa wa Uchaguzi wa TLP unaendelea kufanyika leo, katika ukumbi wa Milleium huko Mbagala, wilayani Temeke ambapo wajumbe na wanachama wa chama hicho watapiga kura kuchagua viongozi wapya.


Wagombea wa nafasi za juu za Uongozi wa chama cha TLP, Joram Kinanda (kushoto) na Mutungirehi wakijadili jambo sambamba na wafuasi wao muda mfupi baada ya kuzuiwa kuingia mkutanoni

No comments:

Post a Comment