Katika tukio la kushangaza wakazi wa eneo la Yombo Vituka, Dar es Salaam Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Barabara ya Mwinyi amefunga milango ya madarasa ya shule hiyo na kisha kutembea mbele.
Sponsor ilitembelea eneo hilo na kukuta vurugu kubwa ya wanafunzi hao huku wakiwa wamebeba bango kubwa likiwa linasomeka 'MKUU HATUTAKI UFISADI UONDOKE, BY WANAFUNZI' huku wakipiga mayowe "Hatukutaki uondoke... tumechoka na mateso yakoo.."
Mmoja wa walimu aliekuwepo eneo hilo la tukio aliiambia sponsor kuwa chanzo kikubwa cha vurugu hizo ni Mwalimu Mkuu kuamua kuwafungia milango ya madarasa wanafunzi hao kwa madai ya kushindwa kulipa baadhi ya michango, ambayo hata hivyo wanafunzi hao walidai ni batili na ya kifisadi.
"Anatulipisha shs 5000 wakati tunatakiwa kulipia shs 200, huyu ni fisadi hatumtaki aondokee..." Alisema mmoja wa wanafunzi hao aliejitambulisha kwa jina la Hamis Mbegu, huku akiwa na jazba.
Juhudi za kumpata mwalimu Mkuu huyo aliyefahamika kwa jina la Hellen Mngoya, zilifanikiwa baada ya Sponsor kutafuta namba zake za simu na kisha kumpigia. Baada ya kumpigia simu na kupokea mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;
Sponsor: Unatuhumiwa na wanafunzi wako kwa ufisadi wa michango na kuwakosesha masomo, unalizungumziaje hili?
Mwalimu: Wewe ni nani kwanza, jitambulishe.
Sponsor: Mwandiishi wa habari, nimekuta vurugu za wanafunzi wako wakidai umewafungia milango ya madarasa kwa sababu unawadai michango, naomba maelezo.
Mwalimu: Mimi nilitoka kwenda kuchukua mitihani, wakati nikiwa nimeshawaruhusu wanafunzi wote. hivyo kilichotokea nyuma sikifahamu.
Sponsor: Wanafunzi wanadai kuwa umewakosesha masomo kwa kuwafungia milango ya madarasa, sababu unawadai michango ambayo wao wanadai ni batili, unasemaje?
Mwalimu: Mimi siwezi kuzungumzia suala hilo, mtafute ofisa elimu ndiye anyejua kila kitu kuhusu shule ile.
Baada ya kumaliza mazungumzo hayo, Sponsor pia ilimtafuta Ofisa elimu wa Wilaya ya Temeke ambaye nae alidai hakuwa na taarifa zozote kuhusiana na vurugu hizo, ingawa ni kweli anafahamu matatizo ya shule hiyo.
Shule hiyo yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha tatu ina jumla ya walimu 13, na ni moja ya shule zilizomo katika mpango wa serikali wa shule za kata.
Wanafunzi wa Shule ya Sekodari Barabara ya Mwinyi, kata ya Vituka wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa kukataa uongozi wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kama walivyonaswa na Sponsor.
No comments:
Post a Comment