Monday, April 13, 2009

Ushindani wa kibiashara unaposhika hatamu

Nilishazoea kuona 'Mteja kwetu ni mfalme' katika hoteli,maduka makubwa na kadhalika. Lakini hili la kwenye vituo vya mafuta sasa inaonyesha ni namna gani dhana ya ushindani katika biashara inavyoanza kuchukua nafasi yake.

Sifahamu kama hiki ni kituo cha mzawa ama mgeni. Lakini yote tisa, kumi ni kufunguliwa kwa milango ya kibiashara Afrika Mashariki ambapo sasa tunaanza kuona uwepo wa baadhi ya makampuni mbalimbali ya kigeni yakishika kasi katika sekta ya biashara hapa nchini.

Nchini Kenya kuna desturi ya kunyenyekea mteja zaidi ukilinganisha na kwetu (Tanzania). Sasa sijui ni utamaduni wao ama ni elimu zaidi ya biashara. Wasiwasi wangu ni kufunikwa kwa kampuni za kizalendo na wageni hawa kwa sababu tu ya unyenyekevu na nidhamu zao kwa wateja.

Changamoto yangu kwa kampuni za wazawa, kubadili mitazamo na fikra za kibiashara kulingana na wakati uliopo sasa.


Mpitanjia akipita jirani na bango la kituo cha mafuta lililo na ujumbe wa kuvutia mteja wa bidhaa hiyo..

No comments:

Post a Comment