SERIKALI imesema haiitambui kampuni ya kupanda na kuvuna fedha (DECI Tanzania Limited) kama ni taasisi inayoendesha shughuli zake kihalali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana, Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo amewaambia waandishi wa habari kuwa Kampuni hiyo ilikujisajili kama shirika moja la kidini la 'Evangelic' kwa ajili ya kutoa huduma za kiroho lakini wameshangaa kuona imejiingiza katika biashara ya upatu.
"Kwanza tangu wameanza kuandikwa katika vyombo vya habari, sijawahi kuona hata sehemu moja iliyoandika kuwa haijasajiliwa na Benki Kuu Tanzania (BoT), Alisema na kuongeza
"Kama serkali tunasema kuwa kampuni hii ilikuwa inaendesha shughuli zake kiujanja ujanja, hivyo hatua kali kwa mujibu wa sheria ya Tanzania itachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha vingozi wake katika vyombo vya sheria." Alisema.
Waziri Mkulo akizungumza na waandishi wahabari leo
No comments:
Post a Comment