Friday, June 18, 2010

JK AZINDUA MITAMBO MIPYA YA KUFUA UMEME NA KUZINDUA MRADI WA MAJI


Mhandisi wa Tanesco mkoa wa Kigoma, Jenkins Matumbo akimwonesha Rais Kikwete jinsi mitambo mipya ya kuzalisha umeme inavyofanya kazi katika chumba maalum cha kuongozea mitambo hiyo muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua mitambo hiyo mjini Kigoma jana.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO mhandisi William Mhando.


Rais Kikwete akimtwika maji Mkazi wa Kigoma Bi.Zainabu Gobela muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa maji ujulikanao kama Mkongoro II mjini Kigoma jana

PICHA ZOTE NA FREDDY MARO

Monday, June 7, 2010

TANZANIA WAUNGANA NA BRAZILI KUPIGA VITA MALARIA

Ujumbe wa Kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria toka nchini Brazili ukiongozwa na andres Sanchez leo umekutana na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kupiga vita ugonjwa hatari wa Malaria, ambapo ujumbe huo ulikula chakula cha pamoja cha mchana na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika hoteli ya Moevenpick, jijini hapa Dar es Salaam.


Kiongozi wa ujumbe toka Brazil, Andres Sanchez (kulia) akikabidhi mpira kwa Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Juma Kapuya

WATANZANIA WAOMBEA NCHI ZENYE MISUKOSUKO

Watanzania wenye imani ya kikristo leo wamekusanyika pamoja kwa ajili ya kufanya ibada maalumu ya kuliombea Taifa hili la Tanzania na mataifa mengine yaliyo kwenye misukosuko, leo jijini hapa kwenye kanisa la Pentekoste, Manzese uanja wa Sifa.

CRDB YAWAKOMBOA WANAFUNZI

Benki ya CRDB leo imekabidhi mabasi matano kwa Serikali kwa ajili ya kubebea wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango wa kupunguza kero ya usafiri kwa wanafunzi hao.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa ngazi za juu serikalini na wa Benki ya CRDB baada ya kupokea mabasi hayo

HUJAMBO MTOTO MZURI?


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsalimia mtoto

MPIGAPICHA MKUU WA HABARILEO AELEZEA AJALI ALIYOIPATA

Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Habari Leo linalochapishwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya (TSN), Athumani Hamisi leo alikutana na waandishi wa habari na wapigapicha katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ulioko katikati ya jiji la Dar es Salaam na kuzungumzia mazingira ya ajli aliyoipata.