Rais Jakaya Kikwete amefanya ziara ya kushtukiza katika Mamlaka ya Usimamizi wa bandari Tanzania (TPA), leo hii na kukutana na lundo la shehena za mizigo bandarini hapo...
Akiwa katika vazi la ki'marekani,' yaani shati, koti na suruali ya jeans, Rais Kikwete alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Ephraim Mgawe kuhakikisha shehena hizo zinapungua haraka iwezekanavyo ili kupisha shughuli nyingine za upakuaji mizigo bandarini hapo...
'Hili gari limeandikwa limetumwa mwaka jana lakini mpaka leo lipo hapa halijaondolewa, tatizo ni nini hasa?" Alihoji Rais...
Na hii hapo chini ilikuwa ni sehemu ya tukio hilo lenyewe, lililomfanya Mkurugenzi huyo wa TPA, kutokwa na jasho kila mara alipokuwa akipachikwa swali na Rais...
Nakukaribisha katika Blogu ya Akida uhabarike kwa habari za Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani zilizotokea na zitakazotokea... 'be the First to know..!
Monday, March 2, 2009
Sunday, March 1, 2009
KAENI MKAO WA KULA NA PICHA ZA JK KATIKA ZIARA TRA...
Leo Rais Jakaya Kikwete anafanya ziara katika Makao makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)... Si mnajua kwamba hawa jamaa ndio washika dau wakubwa wa kodi zetu? Sasa na haya mambo ya Tanesco nagiza la miaka minne, na mambo mengine kadha wa kadha... Kaeni mkao wa kupata mambo... mimi naelekea huko kwenye ziara yake mheshimiwa, nikirudi nawahabarisha na mapicha teeele....
TANESCO KULIKONI TENA?
Hope mko fit wasomaji wa blog hii au vp? Mimi pia namshukuru Mungu kwa kunijaalia uzima na afya. Nisiuweke sana wala nini, ngoja nitomboke sasa...
Wiki iliyopita jamaa hawa wa mambo ya nguvu za nishati (Taa nesco) walisema huenda nchi ikaingia gizani mpaka mwaka 2013, Binafsi ilinishtua tena sio kidogo maana bila umeme hapa mjini mambo mengi hayaendi... hususan sie watu wa kuingia kila wakati kwenye mitandao... inakula kwako kama wanavyosema watoto wa mjini.
Ishu ni kwamba wanasema ongezeko la watumiaji limepiku mahitaji ya hizi Megawatts... Sasa inakuwajekuwaje hapo jamani heu tusaidiane kwa pamoja... Ina maana walishindwa kulielewa hilo mapema kwamba siku hazigandi jamani? Ni jambo ambalo lipo wazi kabisa kwamba nchi na miji yake inakuwa kadiri siku zinavyokwenda, hivyo mahitaji nayo lazima yaongezeke.. si eti jamani!!
Haya Leo limeibuka jingine la Mbunge mmoja hivi kudai kwamba 'hizo ni mbinu za kuwasafisha watuhumiwa wa Richmond... Mh.. hilo nalo neno! Eh, kadiri siku zinavyokwenda tunashuhudia mambo mapya ambayo yalikuwa nyuma ya mapazia...
Mimi nisiongee saaaana.. ila ukumbi nawaachia wasomaji wa blog hii, nanyi mtoe maoni, mtazamo, hata pia kuishauri mamlaka inayosimamia sekta hii nyeti hapa duniani...
Leteni mambo, habari ndio hiyo!

Navutia...
Mimi ni Mwafrika Halisi...!
Hebu nicheki katika pozi la kimama wa afrika... situmii mkorogo wala sipeleki kichwa changu saluni... Hakika navutia..
Nicheki nilivyopozi na Mavazi ya Kindengereko...
Subscribe to:
Posts (Atom)