Sunday, March 1, 2009

TANESCO KULIKONI TENA?

Hope mko fit wasomaji wa blog hii au vp? Mimi pia namshukuru Mungu kwa kunijaalia uzima na afya. Nisiuweke sana wala nini, ngoja nitomboke sasa...

Wiki iliyopita jamaa hawa wa mambo ya nguvu za nishati (Taa nesco) walisema huenda nchi ikaingia gizani mpaka mwaka 2013, Binafsi ilinishtua tena sio kidogo maana bila umeme hapa mjini mambo mengi hayaendi... hususan sie watu wa kuingia kila wakati kwenye mitandao... inakula kwako kama wanavyosema watoto wa mjini.

Ishu ni kwamba wanasema ongezeko la watumiaji limepiku mahitaji ya hizi Megawatts... Sasa inakuwajekuwaje hapo jamani heu tusaidiane kwa pamoja... Ina maana walishindwa kulielewa hilo mapema kwamba siku hazigandi jamani? Ni jambo ambalo lipo wazi kabisa kwamba nchi na miji yake inakuwa kadiri siku zinavyokwenda, hivyo mahitaji nayo lazima yaongezeke.. si eti jamani!!

Haya Leo limeibuka jingine la Mbunge mmoja hivi kudai kwamba 'hizo ni mbinu za kuwasafisha watuhumiwa wa Richmond... Mh.. hilo nalo neno! Eh, kadiri siku zinavyokwenda tunashuhudia mambo mapya ambayo yalikuwa nyuma ya mapazia...

Mimi nisiongee saaaana.. ila ukumbi nawaachia wasomaji wa blog hii, nanyi mtoe maoni, mtazamo, hata pia kuishauri mamlaka inayosimamia sekta hii nyeti hapa duniani...

Leteni mambo, habari ndio hiyo!

No comments:

Post a Comment