Monday, March 2, 2009

JK ATEMBEZA MKWARA BANDARINI...

Rais Jakaya Kikwete amefanya ziara ya kushtukiza katika Mamlaka ya Usimamizi wa bandari Tanzania (TPA), leo hii na kukutana na lundo la shehena za mizigo bandarini hapo...

Akiwa katika vazi la ki'marekani,' yaani shati, koti na suruali ya jeans, Rais Kikwete alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Ephraim Mgawe kuhakikisha shehena hizo zinapungua haraka iwezekanavyo ili kupisha shughuli nyingine za upakuaji mizigo bandarini hapo...

'Hili gari limeandikwa limetumwa mwaka jana lakini mpaka leo lipo hapa halijaondolewa, tatizo ni nini hasa?" Alihoji Rais...

Na hii hapo chini ilikuwa ni sehemu ya tukio hilo lenyewe, lililomfanya Mkurugenzi huyo wa TPA, kutokwa na jasho kila mara alipokuwa akipachikwa swali na Rais...

No comments:

Post a Comment