Saturday, October 3, 2009

SIMBA HAIKAMATIKI, YANGA YAJISOGEZA...

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya soka ya Yanga leo imefuta uteja wa kurambishwa sukari na timu ya Kagera Sugar baada ya kuichapa kwa magoli 2-0katika mechi iliyochezwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba leo, wakati Simba ya Dar es Salaam ambayo inaongoza Ligi ikishinda dhidi ya Moro United kwa magoli 2-1.


Mlinda mlango wa timu ya Moro United, Rajab Masud pamoja na Nahodha wake Wazir Mahadhi wakiangalia mpira ukiingia wavuni kuandika goli la kwanza, huku mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi akijiandaa kwa lolote litakaloweza kutokea wakati wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo

MISS TANZANIA: BADO KUNA TATIZO

Mrembo wa Tanzania 2009 Miriam Gerald amepatikana katika kinyang'anyiro kilichofanyika usiku wa kuamkia leo, jijini hapa Dar es Salaam. Tunaishukuru kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga 'Uncle' kwa kufanikisha hilo, na kuwa na moyo wa kujitolea tangu mbio hizo zilipoanza.

Pongezi hizo ziende sambamba na changamoto katika kamati hii ya Miss Tanzania, ambayo ni tatizo la kujieleza kwa washiriki wetu pindi inapofikia hatua ya maswali. Jana tulishuhudia baadhi ya warembo hao wakishindwa kujieleza vizuri mbele ya hadhira jambo lililopelekea wengine kutoa majibu yasiyoeleweka.

Nampongeza sana Miriam, ambaye ndiye Miss Tanzania 2009, kwa kujieleza vema kwa usahihi hasa alipoamua kutumia lugha ya kiswahili ambayo ndiyo ya Taifa, ambo lililompa uhuru wa kujieleza na kueleweka kwa majaji, na washabiki waliokuwa wamehudhuria mashindano hayo.

Mungu ibariki lugha yetu ya Kiswahuili, Mungu ibariki Tanzania!


Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Beatrice Lukindo (kulia) na mshindi wa tatu Sia Ndasikoi, baada ya kutangzwa washindi wa shindano hilo Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo

Thursday, October 1, 2009

KWA WASOMAJI WA BLOGU HII

Ni muda mrefu sasa blogu yenu muipendayo ya Sponsor haikuwa 'updated' kutokana na sababu za kiufundi zinazoendelea kufanyiwa kazi na mtaalamu wa blogu hii.

Hivyo nachukua fursa hii kuwaomba radhi wasomaji wangu kutokana na usumbufu wowote unaoendelea kujitokeza, lengo ni kuboresha blogu hii ya Sponsor, ili wewe msomaji uweze kufaidika na habari motomoto.

Ahsanteni.

Akida. F. S
Managing Editor,
Sponsor.blogspot.com

KUMEKUCHA SERIKALI ZA MITAA


Wagombea wa nafasi za ujumbe wa serikali ya mtaa wa Kilakala, Yombo, Dar es Salaam wakipunga mikono walipowasili katika ofisi ya serikali ya mtaa kwa ajili ya kuchukua fomu, mapema leo asubuhi. Wa pili kulia ni shangazi yake mimi, Mariam Akida.

Shangazi yake mimi, Mariam Akida akikabidhiwa fomu ya ugombea nafasi ya ujumbe toka kwa ofisa mtendaji wa mtaa wa Kilakala.

BAYPORT YAGAWA JEZI MAMBO YA NDANI


Meneja Masoko wa Kampuni ya Bayport, Ngula Cheyo (kulia) akikabidhi jezi kwa Ofisa Utumishi anayeshughulikia Michezo, Wizara ya Mamabo ya Ndani ya Nchi, Felister Shuli, kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya klabu ya soka ya wizara hiyo, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Michezo wa wizara, Staford Busumbiro.

Wednesday, September 30, 2009

Taifa Queens yawanyima raha watanzania



Wachezaji wa Taifa Queens ya Tanzania wakipambana na wa timu ya Namibia katika mashindano ya kimataifa ya mchezo wa Netiboli yanayoendelea Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Namibia ilishinda 45-40

African Lyon yaitotesha Amnyema Rangers



Mshambuliaji wa timu ya African Lyon akiwatoka mabeki wa Manyema Rangers wakati wa michuano ya ligi ya soka Tanzania Bara katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo. Lyon ilishinda kwa 2-1.