Tuesday, January 5, 2010

CRDB YAZINDUA ATM MOBILE KWA KISHINDO

Benki ya CRDB imezindua Magari mawili Maalum ya Mashine za kutoa na kuweka fedha yaani 'ATM MOBILE" leo jijini Dar es Salaam.

Akizindua magari hayo Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema magari hayo yatasaidia wananchi kuepukana na kufanyiwa uhalifu kutokana na kuwafikia vijijini badala ya wao kufuata huduma hizo mbali na makazi jambo ambalo linaweza kuwahatarishia usalama wao na mali.

'Mtindo wa kubeba fedha kiasi kikubwa nyingi mkononi umeshapitwa na wakati. Siku hizi dunia imebadilika, kule Ulaya ukibeba hela mkononi mamilioni kwa ajili ya kwenda kununua gari ama kitu chochote watu wanakushangaa na kukutilia shaka. Hivyo tutumie mashine hizi kwa ili kuepkuna na kufanyiwa vitendo vya Uhalifu.' Alisema


Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (nyuma akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dk. Kimei (mbele) kuingia kwenye gari maalum la ATM Mobile wakati wa uzinduzi wake jana

Magari Maalum ya ATM Mobile baada ya kuzinduliwa

Msanii, Marlow na kundi lake akikonga nyoyo za watu wakati wa uzinduzi huo...

ANNE KILANGO ATOA TAHADHARI KAMPENI ZA UCHAGUZI 2010

Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ametoa tahadhari kwa watanzania kuwa makini na wachafuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za urais, ubunge na Udiwani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

Mama Kilango amesema kipindi hiki ni kigumu kutokana na kila mtu kutaka kuonekana msafi mbele ya jamii ili akubalike na hivyo kutumia fursa hiyo kwa kuwachafua wengine.

"Wananchi wawe makini katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani." Alisema.

Sunday, January 3, 2010

SHEREHE YA MDAU AMIR MHANDO KATIKA PICHA


Wafanyakazi wa TSN wakiwakilisha ipasavyo katika mpango mzima...

"Ngoja nikutilie msosi wife.. usipate shida eenh! Kama anamwambia vile wife wake..

Braza Michu naye alikuwepo kuwakilisha mpango mzima...

Baraza f naye aliwakilisha ipasavyo na wife wake na mdogo wake Halifa

Na sasa ni mpango mzima wa kukata keki...


Ally Choki naye alikuwepo mradi tu kuhakikisha mchakato mzima unakamilika

Saturday, January 2, 2010

SAFARI YA MWISHO YA SIMBA WA VITA "MZEE RASHID MFAUME KAWAWA' KATIKA PICHA


Viongozi Wakuu wa Nchi wakisubiri kuswalia jeneza la Hayati Mzee Rashid Kawawa

Jeneza likitoka ndani, Vita Kawawa, mtoto wa Mzee Rashid Kawawa akisaidiana na waombolezaji wengine kulibeba

Baada ya kuswaliwa wanajeshi walilipeleka kaburini...

Mzee Warioba ambaye naye ni Waziri Mkuu wa zamani akiweka udongo katika kaburi la Mzee Kawawa
o
Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein naye akiweka udongo kaburini

Na hapa ndipo ikawa mwisho wa Safari ya Simba wa Vita, Hayati Mzee Rashid Kawawa... Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.

Friday, January 1, 2010

MSIBA WA MZEE RASHID KAWAWA KATIKA PICHA


Mwili wake ulianza kwa kutolewa katika chumba cha kuhifadhi Maiti, hospitali ya Jeshi ya Lugalo

Kisha Maofisa wa Jeshi waliupakia katika gari maalumu la wazi kuanza msafara kuelekea Karimjee

Msafara ukielekea katika Viwanja vya Karimjee

Wananchi wakiwa wamepanga foleni kutia saini kitabu cha Maombolezo

Wananchi wakipita kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Hayati, Mzee Rashid Kawawa..

MATUKIO YA MKESHA WA MWAKA MPYA 2010 UWANJA WA UHURU NA MITAANI KATIKA PICHA


He! umenipiga picha wakati nanyonya? Nami nasherehekea mwaka mpya eti..

Usije dhani amelala huyu, anaomba kwa staili yake mwenyewe anayoijua mwenyewe...

Wazee wa Ngwasuma waliwachizisha mashabiki kinoma mitaa ya Kijiji cha Makumbusho pale..

Huyu ni dadapoa ambaye alikutwa akisubiri wateja eneo la Jolly Club mishale ya saa 7.10 hv usiku

"Ahsante Yesu kwa kunifikisha mwaka 2010..." ndivyo anavyoonekana akiomba dada huyu

Eeh Yesu Nakushukuru kwa kunifikisha mwaka mpya wa 2010..." hawa nao pia walikuwepo...

Uwanja wa Uhuru saa 6.00 wote ulilipuka kwa shangwe na vifijo vya mwaka mpya wa 2010

Watu waliselebuka kwa nyimbo mbalimbali za dini kusherehekea mwaka mpya 2010

Mmetuona jameni? Na sisi pia tupo eenh?