Akizindua magari hayo Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema magari hayo yatasaidia wananchi kuepukana na kufanyiwa uhalifu kutokana na kuwafikia vijijini badala ya wao kufuata huduma hizo mbali na makazi jambo ambalo linaweza kuwahatarishia usalama wao na mali.
'Mtindo wa kubeba fedha kiasi kikubwa nyingi mkononi umeshapitwa na wakati. Siku hizi dunia imebadilika, kule Ulaya ukibeba hela mkononi mamilioni kwa ajili ya kwenda kununua gari ama kitu chochote watu wanakushangaa na kukutilia shaka. Hivyo tutumie mashine hizi kwa ili kuepkuna na kufanyiwa vitendo vya Uhalifu.' Alisema

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (nyuma akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dk. Kimei (mbele) kuingia kwenye gari maalum la ATM Mobile wakati wa uzinduzi wake jana

Magari Maalum ya ATM Mobile baada ya kuzinduliwa

Msanii, Marlow na kundi lake akikonga nyoyo za watu wakati wa uzinduzi huo...
No comments:
Post a Comment