Tuesday, January 12, 2010

BREAKING NEWZZZZZZZZ: MAMIA WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA TETEMEKO HAITI

Mamia ya watu wamehofiwa kufa kufuatia tetemeko kubwa lililotokea Haiti. Haiti ni moja ya Kisiwa cha Carribean.
Majengo makubwa yakiwamo Hospitali, Hoteli, Jengo la Benki ya Dunia pamoja na Makazi ya Rais yaliharibiwa vibaya na tetemeko hilo ambalo halijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 200.

Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wanahofia kuwa mamia ya watu hata kufikia maelfu juenda wakawa wamepoteza maisha katika tetemeko hilo lililotokea katika kipimo cha Richa 7.1

Ilichukua takribani saa moja kwa tetemeko hilo kuharibu vibaya eneo kubwa la mji wa Port-au-Prince, uliopo maili 10 kutoka mji mkuu wa Kisiwa hicho


Wakazi wa Haiti wakikimbia baada ya tetemeko hilo

Moja ya gari likiwa limefunikwa na kifusi baada ya tetemeko hilo

SOURCE: SKY NEWS

WANATAALUMA WAZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA KUCHANGIA WAHANGA WA MAFURIKO

Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN) kwa kushirikiana na Mitandao ya www.jamiiforums.com, www.issamichuzi.blogspot.com na Mtandao wa Habari, Burudani na Harakati za Kisiasa wa www.mwanakijiji.com na Push Mobile umezindua Kampeni ya Kusaidia wahanga wa Mafuriko yaliyoikumba meneo mbalimbali ya nchi hapa jijini.

Kwa wale watakaopenda kutoa michango yao kupitia TPN watoe kwa njia zifuatazo:

1. Crossed Cheque, written to: Tanzania Professional Network
2. Bank Deposits or Transfers to: Account Name: Tanzania Professionals Network, Bank Name: CRDB Bank, Bakn Branch: Lumumba Branch, City: Dar es Salaam, Country: Tanzania, Swift Code: CORUTZ TZ, US $ A/C No: 02J1 007 608 900: TZS A/C No: 01J1 007 608 901
2. M-PESA (Vodacom): 0768 777 888
4. Z-Pesa (Zantel): 0773 88 18 88
5. Zaap (Zain) 0784 00 88 99
6. Western Union- Tuma kwa: Mr. Emmanuel Mmari: TPN Finance and Administrative Manager; Dar es Salaam. Tuma Nakala ya MTCN kwa president@tpn.co.tz
7. Fedha Taslimu: Ofisi za TPN- Barabara ya Nyerere: Jengo la TOHS (Dar Group); Ghorofa ya 1, karibu na Radio Tanzania.
8. Kuchangia kupitia makato ya kila siku ya muda wa maongezi: Changia shs 150 kwa siku kwa waathirika wa mafuriko. Tuma sms yenye neno TPN kwenda 15522. Utakatwa shs 250 kujisalili. Kwa Maelezo zaidi wasiliana na 0715 740 047


Mkurugenzi wa Jamii Media inayomiliki tovuti ya Jamii Forum, Maxence Melo (kushoto) akisistiza jambo wakati wa Mkutano na waandishi kuhusu Kampeni hiyo leo Dar es Salaam. Mwingine ni Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), Sanctus Mtsimbe

Monday, January 11, 2010

Wawili wanaswa kufuatia shambulio dhidi ya Togo

Watu wawili wamekamatwa wakihusishwa na Shmabulio dhidi ya Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Togo, Kituo cha Habari cha Angola kimeripoti

Katika shambulio hilo watu wawili walikufa baada ya kushambuliwa kwa risasi katika basi walilokuwa wamepanda kuelekea Angola, katika Mji wa Cabinda, Ijumaa iliyopita.

Watu hao waliokamatwa wakihusishwa na shambulio hilo walikutwa eneo la jirani na shambulio lilipotokea, kwa mujibu wa Radio hiyo.


"Watu wawili wamenaswa. Tutakapokuwa na taarifa kamili tutaitoa kwa wananchi." Mwansheria Mkuu wa jimbo la Cabinda, Angola, Antonio Nito alikiambia kiyuo hicho.

Katika shambulio hilo, Kocha Mkuu Msaidizi wa timu hiyo, Amalete Abalo pamoja na Msemaji wa timu hiyo, Stanislas Ocloo walikufa pamoja na dereva wa basi lililobeba wachezaji ambapo wengine nane walijeruhiwa.

Kikosi hicho sasa kimerejea nyumbani Togo. Wachezaji walitaka kubaki kucheza kwa ajili ya kuomboleza wenzao waliokufa, lakini Serikali ya nchi hiyo ilitoa amri ya kurudi nyumbani kwa timu hiyo.
SOURCE: SKY NEWS


Nahodha wa Timu ya Taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor

Ex-Nazi Officer Jailed For Italy Massacre

A former Nazi has been jailed for life for ordering the massacre of civilians in an Italian village in 1944.

A German court heard how 90-year-old Josef Scheungraber ordered the execution of 10 Italian civilians as a reprisal for the killing of two Nazi soldiers.

A 74-year-old woman and three men were shot dead in the streets of Falzano di Cortona, near the Tuscan town of Arezzo.
German soldiers then forced 11 males aged between 15 and 66 into the ground floor of a farmhouse - and then blew them up.
Only one person survived the massacre, but with serious injuries.

Although 14 civilians were killed, the court only found enough evidence to convict Scheungraber of 10 murders and one attempted murder.
He was dressed in a traditional Bavarian jacket and appeared in good health as he listened to the judgement.




SOURCE: SKY NEWS

KAMATAKAMATA YA VIBAKA NA WAPIGADEBE UBUNGO BUS TERMINAL KATIKA PICHA


Vijana wa Kova wakipita jirani na Kalandinga lililosheheni vibaka na wapigadebe wa Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani ya Ubungo baada ya kukamatwa jana

Mpigadebe/ Kibaka wa Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani ya Ubungo akiingia kwenye Kalandinga huku akimkodolea macho askari baada ya kutiwa nguvuni...

Vibaka/ Wapigadebe wa Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani ya Ubungo wakiingia kwenye Kalandinga baada ya kutiwa nguvuni na vijana wa Kova katika

KONSALT YAZINDULIWA RASMI

Kampuni ya Kizalendo ya Ushauri wa masuala ya kitaaluma ya KONSALT imezinduliwa rasmi.

Akizindua Kampuni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), Emmanuel Ole Naiko amesema kuwa watanzania hawana budi kutumia Kampuni za Ushauri wa Kitaaluma kwa ajili ya kuongeza Ufanisi zaidi.

"Mtu mmoja huwezi kujua kila kitu. Maeneo mengine wape wenzako wenye ujuzi zaidi katika maeneo hayo." Alisema.


Meneja Mshauri wa Kampuni ya KONSALT, Dickson Hyera (kulia) akionyesha sehemu za ndani ya Ofisi ya Kampuni yake kwa Ole Naiko..

Friday, January 8, 2010

TIMU YA TAIFA YA TOGO YATEKWA, YASHAMBULIWA NA WAASI

Basi lililobeba wachezaji wa timu ya Taifa ya Togo kuelekea Angola katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika limetekwa na kushambuliwa na waasi jana Ijumaa, maofisa wa timu hiyo wamesema.

Shirika la Habari la Angola, ANGOP limeripoti kuwa watu 9 walitekwa na waasi hao kwa kutumia bunduki za kivita aina ya AK-47, ambapo nane ni raia wa Togo na mmoja wa Angola.

Mchezaji wa Kimataifa wa timu hiyo anayechezea Klabu ya Nantes, Ufaransa, Thomas Dossevi, ambaye ni mmoja kati ya waliokuwa wametekwa alisema dereva wa basi hilo aliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa shambulizi hilo na wengine watatu walijeruhiwa.

Kikosi cha usalama cha Cabinda cha nchi hiyo, kimelaumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wakati wa tukio hilo.


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Togo..