Friday, January 8, 2010

TIMU YA TAIFA YA TOGO YATEKWA, YASHAMBULIWA NA WAASI

Basi lililobeba wachezaji wa timu ya Taifa ya Togo kuelekea Angola katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika limetekwa na kushambuliwa na waasi jana Ijumaa, maofisa wa timu hiyo wamesema.

Shirika la Habari la Angola, ANGOP limeripoti kuwa watu 9 walitekwa na waasi hao kwa kutumia bunduki za kivita aina ya AK-47, ambapo nane ni raia wa Togo na mmoja wa Angola.

Mchezaji wa Kimataifa wa timu hiyo anayechezea Klabu ya Nantes, Ufaransa, Thomas Dossevi, ambaye ni mmoja kati ya waliokuwa wametekwa alisema dereva wa basi hilo aliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa shambulizi hilo na wengine watatu walijeruhiwa.

Kikosi cha usalama cha Cabinda cha nchi hiyo, kimelaumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wakati wa tukio hilo.


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Togo..

No comments:

Post a Comment