Tuesday, January 12, 2010

BREAKING NEWZZZZZZZZ: MAMIA WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA TETEMEKO HAITI

Mamia ya watu wamehofiwa kufa kufuatia tetemeko kubwa lililotokea Haiti. Haiti ni moja ya Kisiwa cha Carribean.
Majengo makubwa yakiwamo Hospitali, Hoteli, Jengo la Benki ya Dunia pamoja na Makazi ya Rais yaliharibiwa vibaya na tetemeko hilo ambalo halijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 200.

Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wanahofia kuwa mamia ya watu hata kufikia maelfu juenda wakawa wamepoteza maisha katika tetemeko hilo lililotokea katika kipimo cha Richa 7.1

Ilichukua takribani saa moja kwa tetemeko hilo kuharibu vibaya eneo kubwa la mji wa Port-au-Prince, uliopo maili 10 kutoka mji mkuu wa Kisiwa hicho


Wakazi wa Haiti wakikimbia baada ya tetemeko hilo

Moja ya gari likiwa limefunikwa na kifusi baada ya tetemeko hilo

SOURCE: SKY NEWS

No comments:

Post a Comment