Thursday, March 25, 2010

CHINA YAMWAGA PIKIPIKI 100 DAR CITY



Halmashauri ya Jiji la Changzho, China imetoa msaada wa pikipiki 100 kwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia maendeleo katika kata zake.

Meya wa jiji hilo Weng Wengcheng amesema msaada huo ni matunda ya ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili hususan miji hii miwili ya Changzhou na Dar es Salaam.

Miji hiyo ni miji dada kutokana na ushirikiano wa kiuchumi uliopo kati yao.

Monday, March 22, 2010

MVUA, WATOTO NA HATARI BARABARANI



Nimegundua kuwa watoto wenye umri mdogo hasa wale walio darasa la kwanza, hupenda kucheza katika mvua pindi zinaponyesha.

Katika pitapita zangu za kutafuta habari leo asubuhi nikianzia wilayani Kinondoni, Ilala na kumalizia Temeke nimekutana na watoto ambao ni wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya hizo wakiwa vifua wazi huku wakikimbizana katikati ya mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha kwa mafungu jijini hapa.

Nilipigwa butwaa nilipowaona watoto wakikatiza barabara ya Kawawa eneo la Kigogo, wakikimbia pasipo kuangalia usalama wao huku magari yaendayo kasi yakipishana nao.

Hali hiyo ilinistaajabisha na kutafakari kuhusu umuhimu wa wazazi kuchukua tahadhari kwa watoto wao pindi mvua zinaponyesha.

UANDIKISHAJI WAPIGAKURA WAANZA LEO DAR



Zoezi la kuboresha daftari la wapigakura limeanza leo katika vituo mbalimbali vilivyoteuliwa, jijini hapa leo.

Sponsor ilishuhudia maeneo mbalimbali hasa katika shule za msingi kukiwa na mikusanyiko ya wananchi wakijiandikisha katika daftari la wapigakura.

Vituo hivyo ni Hananasif Kinondoni, Basata Ilala na Shule ya Msingi Makamba Temeke.

"Kwa ujumla zoezi limeanza vizuri, wananchi wameitikia wito." Alisema Flora Luhamo, mwandikishaji wa kituo cha Hananasif.

Monday, March 15, 2010

HUU NI UCHIZI AU KUJIENDEKEZA?



Mkazi huyu wa jijini hapa amekutwa na blog hii akikoga maji machafu yanayotoa harufu kali, eneo la Tandika Transfoma jana jioni. Haikufahamika mara moja kama jamaa huyu ni mgonjwa wa akili ama anajiendekeza tu.

Lakini sidhani kama mgonjwa wa akili hukumbuka hata kukoga maji.

Kwa mpango huo basi, hii ni hatari kwa afya yake jamaa huyu.

JK AAPISHA MAKATIBU WATENDAJI TUME YA MIPANGO

Rais Jakaya Kikwete leo amewaapisha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, pamoja na Manaibu Katibu watendaji wanne, Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amemwapisha ndugu Dk. Phillip Isidori Mpango kuwa Katibu Mtendaji wa Tue ya Mipango, Bw. Maduka Paul Kessy kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa tume hiyo pamoja na Bi. Happiness Ngoti Mgalula naye pia kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa tume hiyo.



Wengine ni Bi. Florence Mwanri ambaye ni Naibu Katibu wa Tume hiyo ya Mipango na Bw. Clifford Katondo Tandali naye pia kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo.

Hafla ya kuwaapisha Katibu na Manaibu Katibu wake imefanyika Ikulu, jijini Dar es Salam leo asubuhi.

Friday, March 12, 2010

A NEW DAY HAS COME...

Nine Months have passed, leaving a newly borned baby boy. He's a son of mine. Surely, I'm now joined a wonderful world. The World of a Families.

I'm now called a dadii, compare to the past days. I'm really proud of it! Thank you God for bring me my Lovely SON!

Friday, March 5, 2010

MUHIMBILI SACCOS YAMWAGA VYANDARUA KWA WAGONJWA

Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) kwa wafanyakazi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo kimetoa msaada wa vyandarua 100 vyenye thamani ya sh 580,000/ kwa Mama na Watoto katika hospitali ya Muhimbili.

Msaada huo umekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza Kampeni ya Zinduka, inayopiga Vita Ugonjwa wa Malaria.


Mwenyekiti wa SACCOS hiyo (kushoto) akikabidhi vyandarua hivyo