Tuesday, March 31, 2009

Mazishi ya Marehemu Hamidu Bisanga katika Picha


Waumini wakiswalia jeneza lenye mwili wa marehemu Bisanga kabla ya maziko


Jeneza lenye mwili wa marehemu Bisanga likiwa garini kuelekea makaburini


ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Bisanga kwa ajili ya maziko katika makaburi ya Kisutu..


Safari ya marehemu Hamidu Bisanga ilihitimishwa kwa kuuzika mwili wake katika kaburi hili..
Mungu ailaze roho ya marehemu Hamidu Bisanga mahala pema peponi, Amina!

Mamia wamzika Bisanga

Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam pamoja na maeneo mengine ya jirani, leo wamejitokeza kwa wingi kumsindikiza aliyekuwa mwandishi wa habari wa siku nyingi ndani na nje ya nchi, marehemu Hamidu Bisanga katika nyumba yake ya milele, makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

Marehemu Bisanga alifariki dunia hivi karibuni kwa ajali ya gari, maeneo ya Makumbusho, Dar es Salaam.


Ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu Bisanga wakiwa wamebeba jeneza...

Friday, March 27, 2009

Wezi wa miundombinu ya maji sasa kukiona- DAWASA, DAWASCO

Sasa unaweza kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0756 889 930 pamoja na 0756 444 266, kuitaarifu DAWASCo nani ni mwizi wa miundombinu ya maji. Hii imetokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa miundombinu ya maji hapa jijini jambo linalopelekea wananchi wengine kukosa huduma hii muhimu.


Mkurugenzi wa ufundi wa DAWASA, Boniphace Kasiga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo, kuhusu kampeni kabambe ya wizi wa miundombinu ya maji...

Tuesday, March 24, 2009

SUMATRA YAIPIGA STOP SEAGULL KUSAFIRISHA ABIRIA

Mamlaka ya dhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA), imeipiga stop meli ya Seagull kubeba abiria mpaka hapo itakapokuwa imefanyiwa matengenezo.

Kwa mujibu wa barua yake iliyoiandikia kampuni hiyo, SUMATRA imesema seagull itaendelea na safari zake tu endapo itaridhishwa na maendeleo ya meli hiyo kupitia kwa mkaguzi alieidhinishwa.


Baadhi ya wafanyakazi wa Seagull wakiengalia sehemu ya meli ya seagull iliyoharibika


Meli ya Seagull ikiwa imetia nanga baada ya kuzuiwa kusafiri


Abiria wa Seagull wakirusha chupa za maji baada ya meli hiyo kupigwa stop kusafiri

OBAMA KUZUNGUMZIA UCHUMI WA MAREKANI LEO

Rais Barack Obama wa Marekani leo anatarajia kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mikakati ya maendeleo ya uchumi kwa nchi yake tangu aliposhika madaraka.

PINDA AZINDUA KONGAMANO LA USOMAJI VITABU AFRIKA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo amezindua kongamano la usomaji vitabu kwa nchi za Afrika, leo hapa jijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi amesema kuwa waafrika hususan watanzania hawana budi kusoma vitabu ili kuondokoana na ujinga, umasikini na maradhi.

"Ujinga, umasikini na maradhi pia huchangiwa na kutosoma vitabu." Alisema.

baadhi ya washiriki wa mkutano wa usomaji vitabu kwa nchi za Afrika

Monday, March 23, 2009

Athumani azidi kupata nafuu


Mpigapicha wa magazeti ya Serikali (Dailynews na Habari leo), Athumani Hamisi akionekana mwenye tabasamu pamoja na wafanyakazi wenzake waliokwenda kumjulia hali nchini Afrika ya Kusini.