Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwasili Ofisini kwake leo asubuhi kwa kuanza rasmi kazi.
Nakukaribisha katika Blogu ya Akida uhabarike kwa habari za Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani zilizotokea na zitakazotokea... 'be the First to know..!
Monday, March 19, 2012
MWAKYEMBE AANZA MZIGO RASMI, ASEMA YUKO FITI
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwasili Ofisini kwake leo asubuhi kwa kuanza rasmi kazi.
SHEREHE ZA MIAKA 10 YA NHIF ZAFANA DAR
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akionesha kitabu chenye ripoti ya hali ya afya kwa vijijini baada ya kukizindua wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo, Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), deogratias Ntukamazina.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu, Frederick Sumaye.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (awamu ya tatu), Anna Abdallah.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (awamu ya tatu), Willison Mukama.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Faraja Kihongole.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo, Beda Msimbe.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko kwa mwandishi wa habari wa the Guardian, Joyce Bazira.
Waandishi mbalimbali wa habari wakionesha kitabu chenye ripoti ya hali ya afya vijijini baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokea zawadi maalumu kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Deogratias Ntukamazina.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya akikabidhi tuzo ya shujaa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa mwandishi, Muhidini Michuzi.
SAMIA SULUHU AKUTANA NA VIONGOZI WA WALEMAVU WA MACHO
CHUPUCHUPU...
Mkazi wa Dar es Salaam ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akipepewa baada ya kuzimia kutokana na ajali iliyohusisha daladala lenye namba za usajili T 861BDH inayofanya safari zake kati ya Kisarawe na Buguruni na gari jingine aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 238 BSF, eneo la Kisumu, Pugu, jijini juzi. Hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo. (Picha na Fadhili Akida)
Mtoto akimwangalia Mama yake ambaye jina lake halikufahamika mara moja baada ya kuanguka ghafla na kupoteza fahamu kutokana na ajali iliyohusisha daladala alilokuwa amepanda na gari jingine aina ya Toyota Hilux, eneo la Kisumu, Pugu, Dar es Salaam jana jioni. Hakuna aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.
Wasamari wakiwa wamembeba Mama huyo kumuingiza kwenye gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali.
KAMPENI ZA UDIWANI SONGEA, MWANZA ZAPAMBA MOTO

Mwenyekiti wa chadema Mkoani Ruvuma Joseph Fuime akizungumza jana wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani katika kata ya Lizaboni manispaa ya Songea.

Wafuasi wa chadema mjjini Songea wakimsikiliza mbunge wa chama hicho Chiku Abwao hayupo pichani, jana wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani katika kata ya Londoni mjini Songea.

Mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kata ya Lizabon Alanus Mwanja Mlongo, akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika viwanja vya Londoni mjini Songea.

Mbunge wa viti maalumCHADEMA mh Chiku Abwao akizungumza jana wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya London mjini Songea.
LOWASSA ATEMBELEA SHULE YA ST. ANNE MOROGORO
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro, Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro, Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
Wanafunzi wa Shule ya Sekindari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Mh. Waziri Mkuu Mstaafu.
Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
Friday, February 24, 2012
SUMBAWANGA YAZINDUA KAMPENI YA USAFI ‘SUMBAWANGA NG’ARA’
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akimwongoza Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal katika eneo la mkutano wa hadhara mjini Sumbawanga ambapo alisalimiana na wananchi na badaye alizindua kampeni ya kuuweka safi mji wa Sumbawanga iitwayo 'Sumbawanga ng'ara".
Mama Asha Bilal akimsalimia mtoto Juma Kapele(08) mlemavu wa ngozi 'albino' alipotembelea kituo cha kulelea watotot yatima kinachomilikiwa na kanisa katoliki cha Mtakatifu Martin de Pore kilichpo katika eneo la Katandala mjini Sumbawanga, mtoto Juma alipokelewa mawaka jana na kituo hicho baada ya kutoroshwa na mtu ikidaiwa kwa imani za kishirikina ambapo baada ya siku tatu aliokotwa porini akiwa ametelekezwa lakini alikuwa amepingwa chale mwili mzima
MKuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi vifaa vya usafi Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal ili naye awakabidhi kikundi kinachofanya usafi katika mjini huo wa Sumbawanga muda mfupi kabla dk Bilal hajazindua kampeni ya usafi maarufu kama "Sumbawanga ng'ara"
source: Peti Siyame
Subscribe to:
Posts (Atom)