Monday, March 19, 2012

CHUPUCHUPU...



Mkazi wa Dar es Salaam ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akipepewa baada ya kuzimia kutokana na ajali iliyohusisha daladala lenye namba za usajili T 861BDH inayofanya safari zake kati ya Kisarawe na Buguruni na gari jingine aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 238 BSF, eneo la Kisumu, Pugu, jijini juzi. Hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo. (Picha na Fadhili Akida)


Mtoto akimwangalia Mama yake ambaye jina lake halikufahamika mara moja baada ya kuanguka ghafla na kupoteza fahamu kutokana na ajali iliyohusisha daladala alilokuwa amepanda na gari jingine aina ya Toyota Hilux, eneo la Kisumu, Pugu, Dar es Salaam jana jioni. Hakuna aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.


Wasamari wakiwa wamembeba Mama huyo kumuingiza kwenye gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali.

No comments:

Post a Comment