Sunday, October 31, 2010

BURIANI ELVIS MUSIBA



Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA), Elvis Musiba amefariki dunia leo kwenye hospitali ya TMJ, Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na ndugu wa familia hiyo, marehemu Musiba alikutwa na mauti hayo majira ya saa nne asubuhi hospitalini hapo kutokana na maradhi ya mguu yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Marehemu Musiba alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo ambapo mwezi oktoba mwaka huu alipelekwa nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kabla ya kufikishwa hospitalini hapo Jumamosi ya wiki iliyopita kwa mujibu wa ndugu hao.

Taratibu za mazishi zinafanywa nyumbani kwa marehemu Mikocheni, Dar es Salaam.

Marehemu Musiba katika uhai wake aliwahi kuwa Mtunzi mashuhuri wa simulizi za riwaya ambazo ni pamoja na 'Kufa na Kupona, Kikomo, Kikosi cha Kisasi, Njama na Hujuma na nyinginezo ambapo pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi mbalimbali za wakurugenzi zikiwemo Sematel Ltd (DRC), Exclusive Lodges Resort Ltd, Kamati ya Mahesabu ya Chuo Kikuu cha Ardhi, Akaunti ya Milenia (Tanzania) na Kituo cha Uwekezaji cha TIC.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema Peponi, Amina.

1 comment:

  1. Mungu ailaze mahala pema peponi. Tutamkumbuka sana, pamoja na mengi ni vitabu vyake kama vile njama, kufa na kupona, kikosii cha kisasi nk. Kwake amekufa kiwiliwili lakini kimawazo na kazi zake zitaendelea kudumu daima dumu!

    ReplyDelete