Tuesday, October 27, 2009

TASWIRA KATIKA JIJI...


Haya si mapambo bali ni matambara ambayo yananing'inia katika uzio wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam na kuleta taswira mbaya kwa wageni na wapitao kwa miguu.

Matambara haya ni mabango ambayo muda wake umeshakwisha lakini yameachwa hapa na hatimaye kuraruka na kupeperuka ovyo mithili ya bendera za nchi gani sijui... Haipendezi hata kidogo... Meseji sent!

Swissport wapigwa msasa

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport Tanzania Ltd, waliokuwa wamehudhuria mafunzo ya wiki moja ya Uhakiki wa Uzito waNdege na Mizania, leo wamekabidhiwa vyeti vyao baada ya kumaliza mafunzo hayo.


Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni za Swissport, Mozambique Airlines na Fast Track baada ya kukabidhiwa vyeti vyao leo

Tigo yakabidhi vifaa vya michezo

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ili kuiwezesha timu yake kufanya vema katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shs milioni 6.8 ni pamoja na viatu vya mpira seti 2, jezi za netball 14, track suits jozi 44, jezi za mchezo wa riadha jozi 6, mipira ya miguu 10 na mipira ya pete 5.


Ofisa uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi vifaa hivyo kwa Kamishna Uhamiaji anayeshughulikia Sheria, Wizara ya Uhamiaji na Mambo ya Ndani, Magnus Ulingi

Bunge laanza, Werema aapa


Spika wa Bunge, Samuel Sitta akiongozwa kufungua kikao cha 17 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano, mjini Dodoma jana.

Wednesday, October 21, 2009

RITA WAZINDUA CHETI KIPYA CHA KUZALIWA

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), leo imezindua cheti kipya cha kuzaliwa chenye alama za usalama. Cheti hicho ambacho ni vigumu kughushi kimezinduliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Katiba na Sheria, MAthias Chikawe (kushoto)pamoja na Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko wakibeba mfano wa cheti hicho kipya baada ya kuzinduliwa rasmi leo jijini.

JK AWAAPISHA ALIOWATEUA LEO IKULU


Rais Jakaya Kikwete (mbele katikati), Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein (kushoto) pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioapa jana. Kutoka kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Sazi Salula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Katibu wa Rais, Prosper Mbena na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Christopher Sayi. Waliosimama nyuma ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lyimo.

Thursday, October 15, 2009

Wabunge wachafu kuanza kushughulikiwa

Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM inatarajia kuanza kazi ya kuwachunguza wabunge wenye mienendo isiyofaa katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu wa Kamati hiyo, Pius Msekwa amewaambia waandishi wa habari leo asubuhi wakati wa mkutano na wadau hao wa nyuzi, nyumbani kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.