Monday, April 18, 2011

ZA MWIZI AROBAINI



Wakazi wa Buza Cape Town, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam wakiangalia mwili wa kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Iddi ambaye ni mkazi wa Buza Kinyantira aliyeuawa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi.

Kijana huyo anadaiwa kufumwa akiiba kuku katika moja ya banda la kuku huko Buza, ambapo wananchi hao walianza kukumponda kwa mawe na vitu vizito mpaka kupelekea kifo chake.

Hata hivyo baadaye, askari polisi waliuchukua mwili wake na kwenda kuuhifadhi kwenye chumba cha Maiti cha hospitali ya Temeke jijini, ambapo ndugu zake walikuja kuuchukua kwa mazishi.

PIC/SOURCE: Inno

MARAIS AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA KUJADILI UCHUMI WA AFRIKA

Marais watano wa nchi za Afrika Mashariki leo wamekutana kwa mara ya tisa kujadili maendeleo ya ukuaji wa uchumi kwa nchi zao, kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City, jijini Dar es Salaam leo.

Mkutano huo wa tisa wa uwekezaji barani Afrika umewakutanisha marais, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Mwai Kibaki wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, Dk Ali Mohamed Shein wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Rwanda, Bernard Mukuza.



Marais hao wakiwa kwenye mkutano huo

ZANZIBAR SASA KUPATIWA UMEME WA UHAKIKA UTAKAOPITA CHINI YA BAHARI

Akunti ya Mfuko wa Millennium Challenge Tanzania (MCA-T), leo imetiliana saini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa mradi wa umeme kwa mji wa Zanzibar na Kampuni ya umeme ya India Kalpa-Taru Power Transmission Ltd, jijini Dar es Salaam.

Mkataba huo uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 9 za kitanzania utasaidia ujenzi wa mradi huo utakaoanzia kwenye Kituo cha Ubungo mpaka Ras Kiromoni kwa bara ambapo utapita chini ya bahari na kuibukia Ras Fumba huko Zanzibar kabla ya kuishia kwenye kituo cha Mtoni mjini humo, ukiwa na urefu wa Kilomita 42.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa MCA-T, Bernard Mchomvu (kushoto) akibadilishana hati za mkataba huo na Makamu wa Rais wa Kalpa-Taru Power Transmission Ltd, Vilas Hiremani

DK BILAL ASAINI KITABU CHA RAMBIRAMBI YA MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA BRAZIL

Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal leo ameweka saini kitabu cha rambirambi ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa zamani wa Brazil, Jose Alencar da Silva kwenye ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo, leo jijini Dar es Salaam.



Dk Bilal akisaini kitabu cha rambirambi

MAOFISA WA POLISI NA ELIMU YA KUPAMBAA NA UHALIFU

Programu ya mafunzo ya siku tatu kwa wakuu wa polisi na wilaya nchini katika kubaini, kuzuia na kudhibiti uhalifu kupitia mfumo wa ulinzi ushirikishi imefunguliwa jana mjini Dodoma na kushirikisha maofisa hao kutoka maeneo mbalimbali ya nchi



Baadhi ya maofisa hao wakifuatilia sehemu ya mafunzo hayo

KONGAMANO LA KUPAMBANA NA KUGHUSHI NYARAKA MWEZI UJAO

Kongamano la elimu ya kupambana na ughushi mbalimbali wa nyaraka na fedha haramu kupitia mtandao linatarajiwa kufanyika jijini hapa mwezi ujao.


Mwakilishi wa asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na upambanaji wa matukio hayo nchini, Solomon Njiamoja akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari leo. Mwingine ni Mkurugenzi wa kampuni ya D'Sullivan ya Nairobi, Kenya, Sosthenes Bichang'a.

Friday, April 15, 2011

BATA LA MARIPOTA WA KILI TAIFA CUP SOUTH BEACH LEO

WAANDISHI wa habari za michezo, hususan wa mashindano ya Kili Taifa Cup, leo walikuwa na wakati mzuri ambapo walifanyiwa semina na kisha kushiriki michezo, kula na kunywa, kwenye hoteli ya South Beach, Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Michezo waliyoshiriki ni pamoja na soka kwa mashabiki wa timu mbili mashuhuri za Simba na Yanga ambapo mwisho wa mchezo Yanga waliibuka kidedea kwa kushinda bao moja.

Yafuatayo ni matukio ya bata hilo kwenye picha


Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari


Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Oseah akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya mashabiki wa Simba, .Amri Massare


Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Oseah akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya mashabiki wa Yanga, Muhidin Sufiani


Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe akijibu maswali ya waandishi hao


Waandishi w ahabari za michuano ya Kili Taifa Cup inayotarajiwa kuanza mwezi ujao wakipata darasa