Thursday, February 23, 2012

WAZIRI SAMIA SULUHU ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO ZANZIBAR


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu upakuaji wa makontena katika bandari ya Zanzibar kwa Mkuu wa Mipango (ZPC), Ali Haji Haji wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo mjini humo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Msanifu Haji Mussa na Maofisa wa Bandari ya Zanzibar.




Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samia Suluhu Hassan akitembelea Bandari ya Zanzibar wakati wa ziara yake ya kuangalia shughuli za Maendeleo mjini humo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa bandari, Msanifu Haji Mussa na Maofisa wa Bandari Zanzibar.

Source: VPO

DK BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA CHA MZINDAKAYA


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kuhusu uchinjaji wa ng’ombe na matayarisho yake hadi kufikia nyama kamili kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka, wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt.Mzindakaya, kilichopo Sumbawanga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi naRukwa jana.


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kuhusu vipimo vinavyotumika kabla ya ng’ombe kuchinjwa kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt. Mzindakaya kilichopo Sumbawanga wakati akiwa kwenye ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana.


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kuhusu matayarisho na ufungaji wa nyama katika mifuko tayari kwa kuuzwa kwa wateja kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt. Mzindakaya kilichopo Sumbawanga, wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana.


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi baada ya kuwasili kwenye kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Sumbawanga jana wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa.

Source: VPO

REDDS YATOA ZAWADI ZA WAPENDANAO


Balozi wa kinywaji cha Redds Original Akimkabidhi kifurushi cha zawadi mbalimbali Mkurugenzi wa kampuni ya ASSET Entertainment, Asha Baraka kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wapendanao Duniani.


Balozi wa kinywaji cha Redds Original akimkabidhi zawadi mbalimbali toka Redds, Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania, Angella Msangi kwa niaba ya Uongozi wa Shirika hilo kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Wapendanao Duniani.


Mmoja kati ya Mabalozi wa kinywaji cha Redds Original akimkabidhi kifurushi cha zawadi mmoja kati ya wateja na washirika wa kinywaji hicho hivi karibuni kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Wapendanao Duniani.

Source: Courtesy of Redds Original

Wednesday, February 22, 2012

WAKRISTO NA IBADA YA MAJIVU ST. JOSEPH KUJIANDAA NA PASAKA




Sista Anthonia Samba wa Kanisa la Mt. Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam akiwapaka majivu waumini wa dini ya Kikristo kuashiria Jumatano ya Majivu jijini leo. Waumini wa dini ya Kikristo wameanza kufunga kwa resima kujiandaa na Sikukuu ya Pasaka.

source: Okanda

MAUAJI SONGEA YAFIKIA WATU 10, FFU WAFYATUA RISASI NA MABOMU KUTAWANYA MAANDAMANO


Askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakiondoa mkokoteni uliowekwa barabarani na vijana walioandamana katika eneo la lizaboni Manispaa ya Songea.


FFU wakiondoa magogo yaliyowekwa barabarani na vijana wa lizaboni kupinga wenzao kuuawa na watu wasiojuklikana katika maeneo mbalimbali mjini Songea.


FFU wakiwa na mmoja kati ya vijana aliyeshiriki maandamano haramu mjini Songea kupinga mauaji ya raia yanayoendelea mjini humo ambapo hadi sasa watu 10 wameshauawa na watu wasiojulikana.


FFU wakimshikilia mmmoja wa vijana waliokuwa wakiwarushia mawe katika mapambano kati ya polisi na baadhi ya wakazi wa Songea.


FFU wakiwa na vijana walioshiriki maandamano haramu katika manispaa ya songea kupinga mauaji ya wenzao hasa madereva wa pikpiki yanayoendelea mjini humo.


Mkuu wa Wilaya ya Songea ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo Thomas Sabaya akizungumza wakatika wa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa ruvuma kushoto ni Mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu.


Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Said Mwambungu (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa baada ya kutokea mauaj ya vijana 3 na maandamano kati ya FFU na vijana hao.


Watendaji wa mitaa na Wenyeviti wao wakiwa katika mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Mwambungu wakati wa kikao cha dharura kujadili namna ya kukomesha mauaji ya watu wasio na hatia yanayoendelea katika manispaa ya Songea.

SOURCE: MUHIDINI AMRI/ SONGEA

MUUZA DVD KAMA AL-SHABAAB AU BOKO-HARAM

Huyu si Al-Shabaab wala Boko-Haram, la hasha, ni kijana Idrissa Sadiki Nyambo mkazi wa Mabibo Hostel, jijini Dar es Salaam ambaye ameamua kutoka na ‘staili’ ya aina yake ya kufanya biashara yake ya kuuza dvd.

Idrissa anasema kuwa ‘staili yake hiyo imemfanya apate wateja wengi kwa muda mfupi kwani wateja hao hutaka kujua anabeba vitu gani vya ziada na kwa nini avae hivyo. Ndipo hapo wanapojikuta wamenasa na kuanza kununua dvd zake.


Ustadh Idrissa Sadiki Nyambo akipita kutafuta wanunuzi

Anasema kuwa kwa siku mauzo yake hufikia 50,000/- na wakati mwingine hadi 80,000/-.

Huu ndiyo ubunifu ambao Idrissa Sadiki ameufanya na kujikuta maisha yake yanamwendea vizuri.


Mdau akichagua dvd kwa Ustadh Idrissa Sadiki Nyambo

MBABE ANAPOKUTANA NA MBABE MWENZIE..

Hii ilikuwa mitaa ya Ubungo Riverside jirani na darajani, jamaa anayedaiwa kuwa mbabe wa kuzuia watu kupita njia alipopewa 'kibano' cha haja na mbabe mwenzie baada ya kukerwa na vitendo vyake.

Kamera ya blogu hii ilipofika eneo hilo ilikuta mtifuano huo ambao ulianza kama muvi vile. Jamaa huyo ambaye jina lake halikuweza kupatika mara moja alikuwa akiwazuia watu kupita kwenye 'kamlango' kanakounganisha wakazi wa Ubungo Maziwa na Riverside.

Inadaiwa jamaa huyo alikuwa akimzuia kila anayepita hapo kwa kudai lazima kwanza atandikwe ngumi mbili au tatu hivi (yaani mpitanjia amtandike huyo jamaa) mpaka atakotosheka ndipo amruhusu. Ni jambo la kushangaza kwa kweli, lakini imetokea.

Baadaye vurugu iliibuka baada ya mmoja wa wapitanjia hao kukataa na ndipo 'mbabe' huyo akaanzisha vurugu kabla hajatiwa nguvuni na mbabe mwenzie.

Shuhudia tukio hilo katika picha zifuatazo;


Mbabe (kushoto) akimchimba mkwara mpitanjia sipite kwenye mlango huo


Mbabe mwenzie anatokea na kumtia nguvuni


Mbabe anatiwa nguvuni


Hapa ni kama anamwambia 'ukifurukuta nakutandika ngumi'

source: akidasenior