Saturday, July 31, 2010

REST IN PEACE JENNIFER MWELA....


Bw. Dennis, ambaye ni mumewe marehemu Jennifer akilia kwa uchungu wakati wa kumuaga mpendwa mkewe


Mama wa marehemu Jennifer, Arafa Mgaya naye pia hakuweza kujizuia wakati wa kumuaga mwanaye mpendwa, Jennifer


Na hii ni sehemu ya umati wa watu uliomiminika kumsindikiza Jennifer kwenye safari yake ya mwisho, makaburini Kinondoni leo


Na hapa ndipo safari ya Jennifer ilipokuwa imeishia... Sisi tulimpenda sana, lakini Mungu alimpenda zaidi, Mwanga wa amani umuangazie, apumzike kwa amani...

Thursday, July 29, 2010

SAFARI YA MWISHO YA PRIMTIVA PANCRAS...

Na Primtiva Pancras...,
Hivi ndivyo nilivyozoea kuona BY LINE yake mara kwa mara ninapolisoma gazeti la Mtanzania linalochapishwa na Kampuni ya New Habari.

Ama kwa hakika, 'Prim' kama wengi tulivyozoea kumwita wakati wa uhai wake, alikuwa ni rafiki wa kila mmoja wetu. Hakuna unafiki hapa wa kusubiri mpaka mtu afariki ndo mazuri yake yatangazwe. Kwa aliyemjua 'Prim' hatotia shaka wala kuguna kwa hili nalonena.

Prim, alikuwa hodari wa kazi. Kwa sisi ambao mara moja moja tunakuwa na vijikazi vya hapa na pale, hupenda kuita wanataaluma wenzetu kwa ajili ya kusaidiana. Prim hakusita kuja pindi unapomuita kwenye kazi yako. Na kama hatokuwa na nafasi basi atamtuma mtu mradi tu kazi yako isilale.

Prim ana mengi ya kumzungumzia, ambayo unaweza kutumia siku nzima kuyaandika, lakini kwa kifupi, ndo hayo, Na hii ndiyo Safari ya Mwisho ya Primtiva... Mungu amrehemu sana, Amin.

MAZISHI YAKE PICHANI

Primtiva enzi za uhai wake


Waandishi wakimuaga Primtiva Kanisa la Roman la Hananasif


Mchungaji akifukiza udi kwenye jeneza la Primtiva


Sanduku la Primtiva likishushwa kaburini kwa maziko


Joachim Mushi akimwaga mchanga kwenye kaburi la mke wake, Primtiva

Friday, June 18, 2010

JK AZINDUA MITAMBO MIPYA YA KUFUA UMEME NA KUZINDUA MRADI WA MAJI


Mhandisi wa Tanesco mkoa wa Kigoma, Jenkins Matumbo akimwonesha Rais Kikwete jinsi mitambo mipya ya kuzalisha umeme inavyofanya kazi katika chumba maalum cha kuongozea mitambo hiyo muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua mitambo hiyo mjini Kigoma jana.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO mhandisi William Mhando.


Rais Kikwete akimtwika maji Mkazi wa Kigoma Bi.Zainabu Gobela muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa maji ujulikanao kama Mkongoro II mjini Kigoma jana

PICHA ZOTE NA FREDDY MARO

Monday, June 7, 2010

TANZANIA WAUNGANA NA BRAZILI KUPIGA VITA MALARIA

Ujumbe wa Kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria toka nchini Brazili ukiongozwa na andres Sanchez leo umekutana na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kupiga vita ugonjwa hatari wa Malaria, ambapo ujumbe huo ulikula chakula cha pamoja cha mchana na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika hoteli ya Moevenpick, jijini hapa Dar es Salaam.


Kiongozi wa ujumbe toka Brazil, Andres Sanchez (kulia) akikabidhi mpira kwa Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Juma Kapuya

WATANZANIA WAOMBEA NCHI ZENYE MISUKOSUKO

Watanzania wenye imani ya kikristo leo wamekusanyika pamoja kwa ajili ya kufanya ibada maalumu ya kuliombea Taifa hili la Tanzania na mataifa mengine yaliyo kwenye misukosuko, leo jijini hapa kwenye kanisa la Pentekoste, Manzese uanja wa Sifa.

CRDB YAWAKOMBOA WANAFUNZI

Benki ya CRDB leo imekabidhi mabasi matano kwa Serikali kwa ajili ya kubebea wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango wa kupunguza kero ya usafiri kwa wanafunzi hao.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa ngazi za juu serikalini na wa Benki ya CRDB baada ya kupokea mabasi hayo

HUJAMBO MTOTO MZURI?


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsalimia mtoto