Tuesday, April 13, 2010

DK. MNDOLWA MWENYEKITI MPYA WA BODI BENKI YA KCB TANZANIA

Benki ya KCB Tanzania imepata Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye ni Dk. Edmund Mndolwa ambaye ameshika nafasi ya Mhe. Janet Mbene ambaye kwa sasa ni Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufanyika kwa mabadiliko haya kumezingatia mwongozo wa Benki Kuu ya Tanzania kwa wakurugenzi wa mabenki na taasisi za kifedha wa mwaka 2008 ambao unawazuia wabunge kushika nyadhifa za ukurugenzi wa taasisi za kifedha.



Mwenyekiti mpya wa bodi, Dk. Edmund Mndolwa (kulia) akifafanua jambo

No comments:

Post a Comment