Tuesday, April 13, 2010

ZAIN WAZINDUA SHILINGI 1 KWA SEKUNDE, USIKU SEKUNDE 60

Kampuni ya simu za mkononi ya Zain leo imezindua huduma ya malipo ya shilingi 1 kwa sekunde. Na kwa usiku ni shilingi 1 kwa sekunde 60. Huduma hiyo inafahamika kwa jina la 'Uhuru wa Kuongea'.

Mkurugenzi Mkuu wa Zain, Khaled Muhtadi amesema hiyo ni katika sehemu ya kuboresha huduma za mtandao huo na kuwapa unafuu wateja wake kuweza kumudu gharama za mtandao huo.

'Hii itakuwa ni huduma ya kwanza kwetu kuweza kuwapa unafuu wateja wetu kuweza kumudu gharama za matumizi." Alisema.


Zain officials display billiboards showing 1 tsh tariff 24 hrs

No comments:

Post a Comment