Monday, February 20, 2012

SERIKALI YASAINI MIKATABA MIWILI YA UCHIMBAJI WA GESI NA MAFUTA

Serikali leo imetiliana saini tena Mikataba miwili ya utafutaji wa Gesi na Mafuta katika mikondo inayopita Wialaya za Kilosa, Kilombero na Pangani na Kampuni ya Swala Energy ya Australia.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutiliana saini mikataba hiyo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngelejea amezitaka kila pande kuhakikisha inatimiza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba huo ambapo hata hivyo ameihakikishia kampuni hiyo ya Swala Energy kuipa ushirikiano katika kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.


Waziri Ngeleja akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Waziri Ngeleja amesema mktaba huo ambao utakuwa ni wa miaka 11 umegawanyika katika vipindi vinne tofauti ambavyo amevitaja kuwa ni upanuzi kwa awamu mbili tofauti ambazo ya kwanza itakuwa ya miaka minne na ya pili itakuwa ya miaka mitatu.


Waziri Ngeleja (wa pili kulia) akisaini mikataba hiyo na Mkurugenzi wa Biashara wa Swala Energy, Chris Opperman (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Bodi ya Swala Oil and Gas (Tanzania) Limited, Ernest Massawe


Waziri Ngeleja akibadilishana Mikataba na Mkurugenzi wa Biashara wa SWala Energy, Chris Opperman

Hata hivyo Waziri Ngeleja amewahakikishia wananchi hususani wanoishi jirani na maeneo ya miradi hiyo kunufaika kwa kupata ajira ambazo hata hivyo watendaji wakuu wa kampuni hiyo, Swala Energy wameihakikishia Serikali kuwa asilimia kubwa ya wafanyakazi katika mradi huo itakuwa ni kwa wazawa.

JK AZINDUA MRADI WA SERIKALI WA UWEZESHAJI MIFUGO (SEEDSTOCK) LONGIDO

Rais Jakaya Kikwete amezindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo (Seedstock) kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame katika msimu wa 2008-2009 na 2009-2010 huko Wilayani Longido mkoa wa Arusha.


Rais Jakaya Kikwete akipata dua kutoka kwa mzee wa Kimasai, Mkazi wa Longido, baada ya kupata ulaji wa ng'ombe watano na mbuzi watano toka kwa Rais


Ris Jakaya Kikwete akiteta na Mlemavu wa Macho, Godlisten Ole Olais ambaye anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Longido.

Monday, August 1, 2011

LAGHAI MZOEFU ANASWA MTAA WA KONGO

Usithubutu kusimamisha gari lako pindi akufuatapo na kuanza kukwambia umemgonga! Kitakachofuatia ni kukupora kila kitu kilichomo kwenye gari lako. Huyu ni laghai mzoefu aliyekuwa amefumbiwa macho na wafanyabiashara wa Mtaa wa Kongo jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Nurdin. Lakini waswahili wanasema za mwizi arobaini. Leo amenaswa kweupeee na mgambo wa jiji akitaka kumlaghai dereva wa teksi mtaani hapohapo! Fuatilia tukio zima katia 'series' ya picha


Ilianza hivi... Hawa ni Mgambo wa jiji wapo kwenye Patrol yao...


Ghafla wanamkuta 'Nurdin' akiwa amemzuia dereva wa teksi akidai kagongwa...


Mgambo wanashuka ili kujua nini kinachoendelea...


Mgambo baada ya kuhoji na kuambiwa 'Nurdin' ni laghai na ndio staili zake, wanamkwida na kuondoka naye...


Wanamdhibiti kisawasawa ili kumpandisha kwenye gari lao...


'Nurdin' anapingana nao na kuanza kuleta kashkash...


Lakini nguvu ya 'Teja Nurdin' ni ya kitoto sana kwa mgambo hawa... wanampandisha sasa kwenye gari lao...


Hapa amedhibitiwa kisawasawa akiwa ndani ya gari la mgambo hawa...


Hebu 'cheki' sura hii ukiambiwa ni kibaka na tapeli mzoefu utakataa? Mgambo haoooo wanaondoka na Nurdin...

FOLENI BADO YAWATESA WAKAZI DAR


Magari yakiwayamesongamana kwenye Mtaa maarufu wa Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam kama ilivyonaswa na kamera ya sponsor leo mchana. Foleni ya magari bado ni kero inayowatesa wakazi wa jiji hilo.

FIFA YAENDESHA MAFUNZO KWA MAKOCHA WANAWAKE


Mkufunzi wa mafunzo ya ukocha kwa wanawake wa FIFA kutoka nchini Namibia, Jacqueline Chipanga akielekeza jambo kwa makocha hao kutoka mikoa mbalimbali nchini wakati wa mafunzo hayo yaliyoanza leo kwenye hoteli ya Rainbow, jijini Dar es Salaam.

WASHINDI TIGO JIPANGE KIMAISHA WAKABIDHIWA MILIONI 5


Washindi wa promosheni ya Jipange Kimaisha inayoendeshwa na kampuni ya simu ya Tigo (kutoka kushoto) Festo Saluni, Jane Mtenga na Nasoro Muharam wakiwa wameshikilia hundi yao ya shilingi milioni 5 mara baada ya kukabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.

KOICA YANOGESHA NANENANE MOROGORO


Balozi wa Korea Kusini nchini, Kim Young- Boon (kushoto) akiwa amebeba mgongoni kifaa inachoitwa ‘Jige’ ambacho hutumiwa na wananchi hasa wakulima vijijini nchini Korea Kusini kwa urahisi mara baada ya kufungua Banda la Koica leo mjini Morogoro kwenye Maonesho ya wakulima yaliyoanza kwenye viwanja vya Nanenane mjini humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kanali Mstaafu Issa Machibya.
Picha: John Nditi