Monday, February 20, 2012

SERIKALI YASAINI MIKATABA MIWILI YA UCHIMBAJI WA GESI NA MAFUTA

Serikali leo imetiliana saini tena Mikataba miwili ya utafutaji wa Gesi na Mafuta katika mikondo inayopita Wialaya za Kilosa, Kilombero na Pangani na Kampuni ya Swala Energy ya Australia.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutiliana saini mikataba hiyo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngelejea amezitaka kila pande kuhakikisha inatimiza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba huo ambapo hata hivyo ameihakikishia kampuni hiyo ya Swala Energy kuipa ushirikiano katika kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.


Waziri Ngeleja akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Waziri Ngeleja amesema mktaba huo ambao utakuwa ni wa miaka 11 umegawanyika katika vipindi vinne tofauti ambavyo amevitaja kuwa ni upanuzi kwa awamu mbili tofauti ambazo ya kwanza itakuwa ya miaka minne na ya pili itakuwa ya miaka mitatu.


Waziri Ngeleja (wa pili kulia) akisaini mikataba hiyo na Mkurugenzi wa Biashara wa Swala Energy, Chris Opperman (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Bodi ya Swala Oil and Gas (Tanzania) Limited, Ernest Massawe


Waziri Ngeleja akibadilishana Mikataba na Mkurugenzi wa Biashara wa SWala Energy, Chris Opperman

Hata hivyo Waziri Ngeleja amewahakikishia wananchi hususani wanoishi jirani na maeneo ya miradi hiyo kunufaika kwa kupata ajira ambazo hata hivyo watendaji wakuu wa kampuni hiyo, Swala Energy wameihakikishia Serikali kuwa asilimia kubwa ya wafanyakazi katika mradi huo itakuwa ni kwa wazawa.

1 comment: