Wednesday, February 22, 2012

PINDA AFUNGUA TAWI BARIADI



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh. 5,000,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa CRDB, Tully Mwambapa kwa ajili ya kununualia magodoro na vitanda katika hospitali ya Wilaya ya Bariadi baada ya kufungua tawi la Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga juzi.

source: PMO

ZHAO ZHONGQIU AMUAGA RASMI DK MARY

Aliyekuwa Mwakilishi Mkuu wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania Zhao Zhongqiu leo amemuaga rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu baada ya kumaliza muda wake nchini.


Waziri Nagu akiagana na Zhao Zhongqi


Waziri Nagu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Zhao Zhongqi na Mwakilishi mpya, Lin Zhiyong (kulia)

DK SHEIN AUNGANA NA WAKAZI WA TUMBATU KUADHIMISHA MAULID YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein leo ameungana na wakazi wa Tumbatu, Unguja kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wazee wa Tumbatu mara alipowasili katika bandari ya Kisiwani humo kuhudhuria katika Sherehe za uzinduzi wa Maulidi ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W),yaliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono wananchi waliofika kumpokea wakati alipowasili katika bandari ya Kisiwa cha Tumbatu kuhudhuria katika Sherehe za uzinduzi wa Maulidi ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W),yaliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) pamoja na viongozi wengine na Mashekhe mbali mbali walioalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Maulidi ya Kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W) wakisimama kumswalia Mtume S.A.W wakati Maulidi yakiendelea kusomwa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) pamoja na viongozi wengine na Mashekhe mbali mbali walioalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Maulidi ya Kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W) wakiwa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani,yalimofanyika maulidi hayo.


Ustadh Khamis Kadiru,akisoma Maulid Mlango wa Kwanza,katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani,akiwa na wanafunzi wa Madrasatul Dhuriat Islamia ya Tumbatu katika sherehe hizo za Maulidi ya Kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W), zilizohudhuriwa na waumini wa na wananchi kutoka vijiji mbali mbali jirani na Kisiwa cha Tumbatu.

source: State House/Zanzibar

TRA WAWAPIGA MSASA WAKANDARASI

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) leo imewapiga msasa wakandarasi nchini kupitia chama chao cha Wakandarasi (CATA).

Mwenyekiti wa Bodi ya usajili wa wakandarasi (ERB), Joseph Tango amesema kuwa sema hiyo ina lengo la kutoa elimu kuhusu kodi mbalimbali zinazotozwa na Mamlaka hiyo kwa wakandarasi hao kwa kuwa wao ni walipaji kodi wakubwa nchini.


Ofisa Mwandamizi wa Elimu Mlipakodi wa TRA, Yeremia Mbaghi akizungumza na wakandarasi (hawapo pichani) wakati wa semina hiyo.


Wakandarasi wakifuatilia kwa makini.


Yeremia Mbaghi akiwaongoza Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi, Joseph Tango na Mwenyekiti wa CATA, eng. Davis Baitani kuelekea kupiga picha ya pamoja.


Mwenyekiti wa CRB, Joseph Tango akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CATA, Lawrence Mwakyambiki kabla ya kupiga picha ya pamoja


Mwenyekiti wa CRB, Mwenyekiti wa CATA na Makamu wake, Ofisa Mwandamizi wa Elimu ya Mlipakodi kutoka TRA wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wakandarasi

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA KORONGWEBEACH-WILAYA YA NKASI.

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Mkazi wa Kijiji cha Mwamapuli, Yacoub Jilala ambaye ni mlemavu baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa kijiji hicho alipofika kuzindua ghala la mazao akiwakatika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi, juzi Februari 20, 2012.


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed GharibBilal akikata utepe kuzindua rasmi jengo la bweni la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach iliyopo Wilaya ya Nkasi wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kulia kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.


Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka Jiwe la Msingi katika jengo la bweni la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kushoto kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.

Tuesday, February 21, 2012

HATIMAYE SUGU NA RUGE WAPATANA


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Clouds Media, Rugemalila Mutahaba, wakipeana mikono Dar es Salaam leo kama ishara ya kupatana na kumaliza tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu miaka miwili. Wengine ni wapatanishi wa mgogoro huo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu.

source: anna nkinda

PSPF YATOA MSAADA WA MATAWATI SHULE YA MSINGI BWILINGU CHALINZE MKOA WA PWANI


Kaimu MKurugenzi Ukaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Pensheni wa Utumishi wa Umma (PSPF), Godfrey Ngonyani (kushoto) akikabidhi msaada wa Madawati 60 yenye thamani ya Shilingi Milioni tatu kwa Mjumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani, Jacklin Kitego. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hanifa Kombo.




Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwilingu, Chalinze Mkoa wa Pwani wakibeba madawati kyaingiza madarasani baada ya kukabidhiwa na PSPF leo mjini humo.

SOURCE: MHAMILA