Wednesday, February 22, 2012

DK SHEIN AUNGANA NA WAKAZI WA TUMBATU KUADHIMISHA MAULID YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein leo ameungana na wakazi wa Tumbatu, Unguja kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wazee wa Tumbatu mara alipowasili katika bandari ya Kisiwani humo kuhudhuria katika Sherehe za uzinduzi wa Maulidi ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W),yaliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono wananchi waliofika kumpokea wakati alipowasili katika bandari ya Kisiwa cha Tumbatu kuhudhuria katika Sherehe za uzinduzi wa Maulidi ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W),yaliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) pamoja na viongozi wengine na Mashekhe mbali mbali walioalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Maulidi ya Kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W) wakisimama kumswalia Mtume S.A.W wakati Maulidi yakiendelea kusomwa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) pamoja na viongozi wengine na Mashekhe mbali mbali walioalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Maulidi ya Kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W) wakiwa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani,yalimofanyika maulidi hayo.


Ustadh Khamis Kadiru,akisoma Maulid Mlango wa Kwanza,katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani,akiwa na wanafunzi wa Madrasatul Dhuriat Islamia ya Tumbatu katika sherehe hizo za Maulidi ya Kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W), zilizohudhuriwa na waumini wa na wananchi kutoka vijiji mbali mbali jirani na Kisiwa cha Tumbatu.

source: State House/Zanzibar

No comments:

Post a Comment