Tuesday, March 20, 2012

JK AZINDUA MWAKA WA KIMATAIFA WA USHIRIKA, AZINDUA UJENZI WA JENGO LA USHIRIKA


Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la Ushirika la ghorofa 20. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza (kushoto) na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini (TFC), Hussein Wakasuvi.


Rais Jakaya Kikwete akipewa maelezo na Mkandarasi Mkuu wa ujenzi wa jengo la Ushirika lenye ghorofa 20, Wang Xiangdong wa kampuni ya ujenzi ya kichina (CCECC) inayojenga jengo hilo.

Sehemu ya wafanyakazi wa TFC na Maofisa wengine wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete


Rais Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mwaka wa Kimataifa wa Ushirika, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.


Rais Jakaya Kikwete akipewa maelezo kuhusu miradi mabalimbali inayotekelezwa na wanachama wa Chama cha kuweka na kukopa cha Bandarini Saccos na Mwenyekiti wa chama hicho, Stella Mutayabarwa wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Kimataifa wa Saccos, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo.


Rais Jakaya Kikwete akitazama bidhaa zinazotengenezwa na wanachama wa Chama cha Kuweka na kukopa cha ORWIDO Saccos.


Rais Jakaya Kikwete akitazama bidhaa za nafaka zinazozalishwa na wanachama wa Chama cha kuweka na kukopa cha WANAMA.


Mzuka wa ngoma unapopanda. Msanii wa ngoma akicheza kwa hisia wakati wa sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment